Quantcast
Channel: Siasa Huru
Viewing all 2111 articles
Browse latest View live

Mange Kimambi Aikosoa Ziara ya January Makamba Studio ya Wasafi Records, Adai Ameenda Kumpoza

$
0
0
Siku kadhaa zilizopita Mh January Makamba alitembelea Studio ya Wasafi inayomilikiwa na Msanii Diamond Platnumz, Watu mbali mbali wametoa maoni yao akiwemo na Mange Kimambi ambaye ameandika haya hapa chini kuhusu ziara hiyo:

Mangekimambi_
"Kwanza nianze Kwa Kusema this is not about Diamond, it's about viongozi wasiojielewa . So watu wa mateam mkileta viranga ni block tu.

Naomba kuuliza Waziri wa mazingira anafanya nini ofisi Za WCB??? kulitokea tetemeko huko WCB? Au vyoo vyao vimeziba kutokana na mazingira? Au??? Mara 100 ingekuwa Nape, tungemchamba nae Ila angalau yeye ni department yake, Makamba anahusika vipi na studio za wanamuziki wa Tanzania??? Kama anaweza kuacha kazi Za wizara yake akaenda kuuza sura mtaani why asiende sehemu ambazo wanyonge wanateseka? Why asiende Muhimbili akawaone wale ndugu Za Wagonjwa wa mikoani wanaolala barabarani nje ya hospitali?? why asiende ocean road akaone watanzania wanavyokufa Kwa kukosa huduma sababu hospitali ni ndogo Na wagonjwa ni wengi, Kila Mwaka watanzania 20,000 wanaachwa wafe Na cancer bila kupata mionzi sababu hospitali haiwezi kuhudumia watanzania Wote, why asiende huko? Hii Ndo serikali ya kutetea wanyonge?

Ngojeni niwaambie kilichompeleka January Makamba ofisi za WCB. Kaenda kichama Kama CCM , Yani Huyu kiongozi hayuko Kwa ajili ya kusaidia watanzania yuko Kwa ajili ya Chama tu. Same way Na Nape Kila nachofanya ni Kwa Akili ya Chama sio watanzania, Kilichompeleka January WCB ni Diamond kuichana serikali kwenye radio last week. Diamond alikaliwa shingoni na TRA alipe kodi ya milioni 236.Akawa anasema hana, Diamond akaenda kwa Kikwete, Ndo ile Safari na vijana wake walivyoenda nyumbani kwa JK, walikuwa wameenda kumuomba Kikwete awaombee kwa Magu wasilipe hiyo kodi au ipunguzwe, Kikwete akasema Hapana hawezi kuwaombea. Ndo Dai ikabidi achukue mkopo kiasi akachanganya na pesa zake ndo akalipa Hiyo kodi.Baada ya kulipa Hiyo kodi ndo Dai mapovu yakawa yanamtoka balaaaa kuhusu serikali na makodi, Ndo mpaka last week akawachana mbayaaa kwenye radio. Unaambiwa Dai kaongea kishenzi akawa anasema hawasupport tena CCM Ndo mnamuona January huyo mbiooo kaenda kuua sooooo maana wasije kumpoteza Diamond kwenye Kampeni ya 2020.Dai Alisema kabisa redioni anatamani mpaka ahame Chama, ndo CCM wanamlambalamba asiende upande wa pili, nahisi next time itabidi wamsamehe kodi maana kajua kuwatetemesha, mpaka Waziri wa mazingira kaenda studio za mziki"Amedika Mange Kimambi katika ukurasa wake wa Instagra,

Wananchi Wajichukulia Sheria Mkononi Waua Mtu Mmoja Aliyedaiwa Kuwa Ni Panya Road Mbagala Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
WANANCHI wa Mbagala sabasaba wamemuua kwa kumshambulia kwa mawe na kisha kumchoma moto kijana mmoja anayedaiwa kuwa ni mharifu wa kundi la panya road ambaye alikuwa na wenzake zaidi ya 15 ambapo wawili kati yao walipoteza fahamu kutokana na shambulio hilo.

Tukio hilo la kushambuliwa kwa panya road hao lilitokea majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mbagala Sabasaba baada ya vijana hao kukurupushwa walipokuwa wakikimbia walipokuwa wakifanya uhalifu maeneo ya sabasaba Magengeni na Mbagala Zakhem.

Polisi waliofika eneo la tukio walilazimika kutumia risasi za moto kuwatawanya wananchi ili waweze kuuchukua mwili wa kijana huyo ambaye hakufahamika jina lake.

Akizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Khalfan alisema usalama wa wananchi upo mashakani kufuatia kundi hilo la panya road.

"Hawa panya road walikuwa zaidi ya 15 wakitokea Mbagala Zakhem ambako walikuwa wakikimbizwa na wananchi baada ya kufanya uhalifu na walipofika hapa Sabasaba walizingirwa na wananchi ambapo watatu kati yao walianza kushambuliwa na mmoja kupoteza maisha baada ya kuchomwa moto " alisema.

Wananchi wakiangalia mwili wa kijana anayedaiwa kuwa ni wa kundi la kihalifu la panya road aliyeuawa baada ya kufanya uhalifu maeneo ya Mbagala Zakhem Dar es Salaam leo jioni. Katika tukio hilo vijana wengine wawili walipoteza fahamu kutokana na kipigo cha wananchi.

Rais Magufuli Ameanza Kuirejesha Nchi Katika Misingi yake - Askofu

$
0
0
SIKU moja baada ya viongozi mbalimbali akiwemo Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi kuonya nchi kupoteza mwelekeo miaka 17 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imeelezwa kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli ameanza kurejesha misingi hiyo.

Mwinyi na viongozi wengine akiwemo pia Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba wakizungumza kwenye midahalo ya Kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere juzi, walieleza shaka juu ya nchi kuanza kumeguka katika misingi ya ukabila na udini, hatua waliyosema inatishia umoja na mshikamano wa kitaifa.

Akizungumzia hofu hiyo jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Jamii kwa Madhehebu ya Dini nchini, Askofu William Mwamalanga alisema Rais John Magufuli ameanza kuirejesha nchi katika misingi yake.

“Ni vizuri kueleza hofu iliyopo lakini ni vizuri zaidi kutambua jitihada zinazochukuliwa na Rais wa sasa Magufuli katika kurejesha nchi katika misingi ya Azimio la Arusha ambayo iliweka misingi ya uongozi. “Hili lipo wazi, Mwalimu alikemea rushwa na watu waliogopa rushwa sawa na sasa ambapo hofu ya rushwa ipo tofauti na ilivyokuwa hapo katikati. Rais Magufuli amechukua hatua nyingi kama kuhimiza uwajibikaji na kukemea matumizi mabaya ya madaraka kama ilivyokuwa wakati wa Mwalimu,” alisema Askofu Mwamalanga.

Alisema mbali ya kurejesha misingi ya uongozi, Rais Magufuli pia ameweza katika kipindi cha muda mfupi kujenga heshima ya nchi ya Tanzania nje, kutokana na na jitihada zake za kutetea wanyonge, kuheshimu utu wa mtu, kuhamasisha umoja na mshikamano, kukemea rushwa, kulinda maliasili za nchi, kuhamasisha nchi na Mataifa ya Afrika kujitegemea na kukataa misaada yenye masharti yasiyo na staha kwa Taifa kama alivyofanya Mwalimu Nyerere.

“Ukiangalia kwa makini ni sawa na kusema Rais Magufuli amerithi utashi wa kisiasa wa Mwalimu Nyerere, nionavyo ni vema tukazitambua jitihada anazozifanya katika kuziba nyufa zilizoainishwa na viongozi wetu wakati wa Kongamano la Mwalimu,” alisema.

Aidha kiongozi huyo wa dini alisema Rais Magufuli ameanza kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti ukabila na udini na kuhamasisha umoja wa kitaifa, ikiwa ni pamoja na kujaribu kuondoa pengo kubwa lililojengeka kwa miaka kadhaa baada ya kifo cha Nyerere baina ya tabaka la watu wenye nazo na wasio nacho.

“Ukubwa wa pengo la kipato kati ya wenye nacho na wasio nacho ambao ulikuwa umekua kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni sasa umeanza kupungua. Ni imani yangu kwamba miaka michache ya uongozi wa Rais Magufuli, watu wataheshimiana na kuwa wamoja kutokana na kugawana sawa rasilimali za Taifa,” alisema.

Habari Leo

Wafanyakazi wa TRA na TBS Waliopitisha Makontena 100 Bila Kukaguliwa Watakiwa Kujisalimisha

$
0
0
Serikali imewataka baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) walioshirikiana na wenzao wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitisha makontena zaidi ya 100 bila kukaguliwa na shirika
hilo katika Bandari ya Dar es Salaam kujisalimisha haraka.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw.Charles Mwijage alitoa agizo hilo mwishoni mwa juma wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo.“Nimeanza kukusanya orodha ya majina ya watu waliosaidia kupitisha makontena haya na nikija nayo hawatapona,” alisema.

Aliwataka wote wanaojijua kuhusika kujisalimisha mapema na kutubu ili wasamehewe kabla haya hatua hiyo.Makontena hayo yalipitishwa katika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni bila ya kuthibitishwa na shirika hilo.

Pia aliitaka TRA kuacha kutoa makontena bila ya shirika hilo kuthibitisha au kukagua ubora wa bidhaa zinazoingizwa hapa nchini sababu mwenye mamlaka hiyo ni TBS.

Alisema watakaotubu kuwa walishiriki waseme walishiriki vipi na lini, walishirikiana na nani na wataje sehemu yalikopelekwa makontena hayo ili serikali iweze kusaidia kukomesha hali hiyo.Alisema anaamini kuwa waliofanya hivyo katika mamlaka hiyo walifanya kwa utashi wao bila ya ushiriki wa viongozi wao na kwamba sasa wakati umefika wa kukomesha tabia hiyo.

Alilitaka baraza hilo kushirikiana na menejimenti na kuhakikisha matatizo yanayojitokeza yanapatiwa ufumbuzi kwa maslahi ya nchi na kwamba serikali itahakikisha inaongeza vitendea kazi na watumishi ili kufikia malengo ya shirika.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Egid Mubofu, baraza hilo lina wajumbe 48 wanaotoka katika vitengo mbalimbali na litakaa kwa muda wa miaka mitano.“Baraza hili linaundwa kutokana na mkataba wa menejimenti na Chama cha Wafanyakazi (RAAWU),” alisema Dkt. Mubofu na kuongeza kuwa menejimenti itashirikiana na baraza kufanyakazi za shirika kwa tija.

Alisema wafanyakazi wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu katika majukumu yao ya kila siku.Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi (TBS), Prof. Mekanya Maboko alilitaka baraza hilo kufanya kazi kwa kushirikiana na menejimenti na bodi kuhakikisha shughuli za udhibiti wa ubora zinafanyika kwa ufanisi.

“Bodi itaendelea kuisimamia menejimenti na kuishauri ifanye kazi kwa kuzingatia sera na sheria,” alisema.

Said Aliyetobolewa Macho Akabidhiwa Bajaji Mbili Zingine Mpya

$
0
0
Waumini wa Dini ya Kiiislam wa madhehebu ya Bohora kupitia kwa Kiongozi wa Mkuu Saydina Dr.Muffaddar Saifdeen wametoa Bajaji mbili mpya kwa Kijana Said Ali Mrisho ambaye alijeruhiwa Hivi karibuni na kupoteza macho yote mawili ikiwa ni mwitiko wa Mkuu wa Mkoa wa dsm kuwaomba wananchi wenye uwezo kumsaidia kijana huyo.

Msaada huo wa bajaji mbili ambazo atazifanyia biashara ili zimuongezee kipato zilikabidhiwa kwa Mkuu wa mkoa wa Dsm paul makonda ambaye pia alizikabidhi kwa said katika hafla iliyofanyika katika msikiti wa Bohora Uliopo Upanga jijini dsm.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul makonda akizungumza na waandishi wa habari amesema jamii na watu mbali mbali wenye Huruma wamendelea kujitokeza kusaidia kijana saidi ambaye haoni kabisa,huku akiwa na familia inayotegemea wakiwemo watoto wawili,mke pamoja na mama yake mzazi.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Bw,Said ambaye hivi sasa ni mlemavu wa macho ameshukuru vyombo vya habari katika kufichua habari zake lakini shukran za kipekee amezipeleka kwa Mkuu wa mkoa wa dsm ktka kumsimamia mpaka jamii imeanza kujitokeza kumsaidia.

Kijana Said ali alipoteza macho yote mawili baada ya Mtuhumiwa Njwele Maarufu Scorpion ambaye hivi sasa yuko rumande baada ya kufikishwa mahakamani kumshambulia kwa visu na kumtoboa macho mwezi mmoja ulipita maeneo ya buguruni mnyamani.

Video: Mrembo Atinga Global Afichua Siri Za ‘Scorpion’

$
0
0
Mrembo aitwaye Talta Msofe (21) akiwa katika pozi baada ya kutinga katika ofisi za Global Publishers kufichua siri za mtuhumiwa huyo, Salum Njwete ‘Scorpion’, mkazi wa Yombo Machimbo jijini Dar es Salaam.

Tazama hapa video Akifunguka

Makamba Aagiza Watu Kuondolewa Mara Moja Katika Chanzo Cha Maji Morogoro

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, January Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, John Mgalula kuhakikisha kuwa ifikapo Novemba 30 mwaka huu watu wote wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu katika chanzo cha maji cha Mambogo waondolewe haraka.

Waziri Makamba alitoa agizo hilo leo wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Mambogo kinachotegemewa na wananchi wa Manispaa ya Morogoro mara baada ya kujionea uhalibifu unaoendelea kufanywa na wananchi hao na kusababisha maji kukauka.

Waziri huyo alimtaka mkurugenzi huyo kuwaondoa na kuwafikisha mahakamani wale wote waliochepusha maji kutoka katika chanzo hicho kwani wamekuwa wkaifanya hivyo kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizopo zinazokataza kufanyika kwa shughuli zozote za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.

Shirika la Ndege Kenya Laahirisha Safari zake, Wafanyakazi Wagoma

$
0
0
Shirika la ndege la Kenya Airways limeahirisha safari zake tano za kwenda ndani na nje ya nchi leo October 16 2016 kutokana na upungufu wa Wahudumu wa ndege kazini.

Taarifa inasema sababu hasa ya kuahirisha safari hizo tano za Mombasa, Kilimanjaro, Juba, Maputo, Harare na Lusaka ni kutofika kazini kwa Wahudumu wa ndege ambao wamepangiwa zamu kwa wakati huo.

Imeelezwa kuwa baadhi ya Wafanyakazi wa shirika hilo hawajaripoti kazini toka Ijumaa iliyopita ambapo shirika linaendelea kufatilia kujua chanzo ni nini na jinsi ya kutatua tatizo na Mwajiri.

Kwa utaratibu ndege za abiria huwa na masharti yake kwenye kila safari ikiwa ni pamoja na kuwa na namba flani ya idadi ya Wahudumu ndani ya ndege ambayo ni lazima itimie, sasa kutokana na Wahudumu wa Kenya Airways kuwa wachache imebidi ndege nyingine zisisafiri.

Wazazi na Walezi Mnayajua Lakini Wanayoyafanya Watoto Wenu?

$
0
0
Leo nilikua naomba kuwauliza walezi na wazazi wenzangu ambao tunalea watoto na tunaishi majumbani mwetu kama tunakua na ukaribu na watoto wetu ili kujua changamoto wanazopitia haswaa mashuleni na mitaani!

Kwa sababu niseme tu ukweli watoto wetu wenye rika la miaka 13 hadi 19 wengi ni shida wawapo mashuleni!

Nyumbani anaweza kuonekana mtiifu,mnyenyekevu na bonge la mstaarabu mpk mzazi au mlezi ukawa unajisifu Ila huku shuleni sasa ni mtukutu,kiburi na wanaume pia anao km ni wa kike...

Kama wa kiume ukute ni mwizi kabisa na bangi anavuta!

Walimu Mara nyingi ndo wamekuwa watu wa karibu na wanaowafahamu vizuri watoto wetu kwa undani kwa sababu muda wa Masaa karibu kumi wanakua nao mashuleni!

Kuna siku nililetewa kesi ya kimapenzi ya mtoto wa kidato cha 3 anajihusisha kimapenzi na mbaba mtu mzima mfanyakazi wa bandarini..

Daah!tulivyomuita kumhoji yule msichana alikiri mpk gesti wanayokutana,simu aliyomnunuloa Samsung S4!

Tulivyomuita mzazi wake alilia sana yule mama..akasema walimu mie Mara nyingi nakua nasafiri kikazi hvyo namuacha peke yake na mwenziwe wa kidato cha NNE!

Kesi nyingine mtoto wa kiume anajihusisha na ubakaji na ameshawahi kubaka mwanafunzi wenziwe.

Mzazi alivyohojiwa anadai yy Mara nyingi anakua bize na maisha mtoto anamuona wikiendi tu!

Kuna kesi nyingine ya tatu

Kabinti kadogo cha 16 kalikua kanaaga kanakuja shule kumbe hakafiki kanaenda kwa mbaba mmoja mkewe alisafiri anakaingilia mwisho wa siku familia inakuja kufahamu kua mtoto hafiki shule,kuhojiwa akasema ukweli.

Wakaazimia akapimwe mimba na HIV..Sad part ni kua binti hakukutwa na mimba Ila alikua ameathirika na kwa maelezo ya mtoto yule mwanaume ndo alikuwa mwanaume wake wa kwanza!
Na alizaliwa mzima kabisa bila HIV

Ushauri wangu kwa wazazi:jitahidini sana kua karibu n watoto wenu,muwafatilie hata km changamoto za kimaisha ni nyingi Ila watoto wetu ni hazina na baraka pekee kutoka kwa Mungu!

Inauma sana kuona kabinti ka miaka16 kameharibikiwa Ila ukianzia chanzo ni wazazi na walezi kutokuwa na ukaribu na watoto wao!

Tukumbuke Tusipoziba ufa mapema tutajenga ukuta!

DC Polepole Awakunjulia ‘Makucha’ Viongozi CCM

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hamphrey Polepole amewapiga marufuku wajumbe wa mashina na viongozi wengine wa  CCM kujihusisha na uidhinishaji  mauzo ya ardhi, huku akiwataka wananchi kuwa makini na kufuata utaratibu wa kisheria wakati wa ununuzi.

Polepole alitoa onyo hilo jana wakati wa mkutano na wakazi wa King’azi Juu, Kata ya Kwembe, baada ya kuelezwa kuwa wana matatizo mengi ya ardhi yanayotokana na baadhi viongozi kuuza eneo kwa mtu zaidi ya mmoja.

Wananchi hao walimweleza kuwa, udanganyifu unaofanyika unatokana na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa na wajumbe wa mashina wa CCM kula njama na wamiliki wa maeneo, kuuzia watu eneo moja zaidi ya mara moja.

Polepole alisema CCM ipo kwenye harakati za kujijenga, hivyo lazima kumaliza migogoro hiyo kama sehemu ya kujirekebisha. Mwenyekiti wa mtaa huo, Seleman Bheho alisema mwaka 2014/15 alipoingia madarakani .ofisi yake ilikuwa akipata kesi za za ardhi nane mpaka 10 kwa siku, lakini sasa zimepungua hadi tatu kwa wiki.

Afande Aitolea Ufafanuzi Picha Aliyopiga na Makamu wa Rais Samia Baada ya Watu Kudhani Ameondoka ACT

$
0
0
Kitendo cha Afande Sele kupiga picha weekend hii akizungumza mbele ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan mkoani Morogoro, kiliibua tetesi katika mitandao ya kijamii zikidai huwenda mwanachama huyo wa ACT amekitosa chama hicho.
afande
Afande Sele akiwa mbele ya msafara wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan

Mwanahiphop huyo ambaye aligombea ubunge katika uchaguzi uliyopita kupitia ACT Wazalendo, wiki moja iliyopita alionyesha kutoridhishwa na mwenendo wa chama chake.

Jumamosi hii baada ya watu kuona picha hiyo na kudhani amekitosa chama cha ACT, aliandika

Aisee Watanzania sisi wengi wetu hata sijui nani katuloga kiasi cha kufunga kabisa uwezo wetu wa kufikiri nakushindwa kutofautisha hata vitu vidogo na vya kawaida sana vinavyotokea ktk maisha yetu ya kila siku…hebu tazama hiyo picha utaona mimi nipo na makamu wa rais,mkuu wa mkoa wetu na viongozi wengine wa serekali,hiyo inamaanisha kwamba hapo niliitikia wito wa serekali sio wito wa chama chochote cha siasa kitu ambacho hata viongozi au wabunge wa upinzani hufanya hivyo kwasababu serikali na viongozi wake ni mali yetu sote kama raia wa Tz sio mali ya chama fulani hata kama viongoz hao wametokana na chama hicho lkn wakishachaguliwa na wananchi wakapewa dhamana ya kuongoza tayari wanakua ni viongoz wa watu wote ktk taifa sio viongozi wa watu wa chama chao tu,sasa nashangaa pale mtu mmoja kwa sababu ya uvivu tu wakufikiri au labda kwa makusudi tu anaamua kuambukiza uvivu wake huo wa kufikiri na kutofautisha mambo kwa watu wengine…mimi nimeitikia wito wa serekali’mamlaka’ninayoamrishwa kuyatii hata ndani ya vitabu vitakatifu sio chama…lkn pia ktk hali ya kawaida tu ninani mwenye utimamu wa akili ktk taifa lolote awezae kukaidi wito wa makammu wa rais ambae ni sawa na rais wa taifa lake?lkn hata kama ingekua kweli mimi nimehama chama ingawa sifikirii kufanya hivyo bado yangebakia kuwa ni maamuzi yangu na yangepaswa kuheshimiwa…nyongeza ni kwamba hata yule mgombea urais wa marekani kupitia chama cha Republican mr donald trump siku za nyuma alikua ni mwanachama mtiifu wa chama cha mpinzani wake bibi clinton cha democratic na maisha yanaendelea..watz tujifunze maana ya maisha halisi tusijenge taifa la uzushi,fununu na kupakaziana…muwe na j’pili kareem akina ndugu nyote!

Niliingia Kwenye Muziki Bila Kupanga – Nick wa Pili

$
0
0
Muziki ulimvuta Nick wa Pili aufanye kwakuwa yeye hakuwa na habari nao kabisa.

Rapper huyo amedai kuwa hata wimbo wake wa kwanza redioni ulitoka bila yeye kupanga.

“Mimi ni mtu ambaye sikuwahi kustruggle kurekodi au kutafuta kutoka. Hata wimbo wa kwanza kusikika redioni ulikuwa ni by default,” Nick wa Pili alieleza kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir.

“Nilikuwa natoka Mwenge naenda Mabibo and then Joh Makini alikuwa anaenda all the way studio, tulivyofika pale river side akasema ‘hebu na wewe tembelea studio uone kinatokea nini.’ Wakati yeye anaandaa verse zake pale, mimi nikawa nimeingia booth nikawa kama nafreestyle yaani kupass time. And then nilipotoka nikakuta watu wote kule studio wakiwa wamesimama, walikuwa wamerekodi zile freestyle, so they want to keep it iwe verse. Nikasema ninaweza kufanya kingine zaidi ya hicho,” aliongeza.

“So from there pressure ya marafiki na nini na mafans nilikuwa nimeshapata so ikabidi niendelee.”

Katika hatua nyingine Nick alikiri kuwa kwa upande wa kipaji ukiwalinganisha na Joh Makini, kaka yake anamzidi mbali.

“Joh Makini ana experience kuliko mimi halafu naweza kusema in terms of music yeye ana ujaribu mkubwa kuliko mimi, yeye amethubutu vitu vingi ambavyo naweza kusema mimi baadaye nikaweza kufaidika kupitia hivyo vitu. Nadhani Joh Makini will all due respect talent wise amenipita mbali kwa mimi ninavyotizama.”

Lowasa Jifunze kwa Dr Slaa

$
0
0
Dk Willibrod Slaa aliposhawishiwa kugombea urais mwaka 2010 alipokuwa Chadema, alipambwa na kila aina ya sifa. Hata baada ya kushindwa, walimwita rais wa mioyo ya Watanzania.

Chadema walimwonesha Dk Slaa mapenzi makubwa na yeye aliyaona. Mwaka 2015 walitofautiana, Chadema haohao walimwonesha chuki kubwa na yeye aliiona.

Walipompenda walimwita Rais wa Mioyo ya Watanzania, walipomchukia walimwita msaliti, mwanaume anayetawaliwa na mkewe, vilevile aliyehongwa mabilioni na CCM.

Ngoja nikwambie; Mapenzi ya wanasiasa wa Chadema kwa Slaa yalikuwa ya fursa. Hayakuwa mapenzi ya moyoni. Ndiyo maana kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015, walimfanyia mabadiliko (sub) ya juu kwa juu, baada ya kuona usajili wa Edward Lowassa kutoka CCM, ulikuwa fursa kubwa zaidi.

Lowassa alibeba matumaini makubwa ya Chadema pamoja na vyama vya Cuf, NCCR-Mageuzi na NLD kupitia muungano wao wa Ukawa, kwa hiyo yeyote yule ambaye alikuwa anaenda kinyume naye kwenye vyama hivyo, alijikuta akiumizwa vibaya.

Kama Prof Ibrahim Lipumba ndivyo ilivyo kwa Dk Slaa, walipendwa kwa fursa na wametoswa kwa sababu ya fursa kwa Lowassa. Siku Lowassa naye ataonekana siyo fursa, mapenzi yatakoma au kuhamia kwa mwingine.

Lowassa alikuwa na watu wengi CCM lakini alihama na wachache, ni kwa sababu aliokuwa nao CCM waliamini ni rais ajaye, kwa hiyo wakampenda kwa kumuona ni fursa yao.

Waliobaki CCM na kumuacha Lowassa akihamia Chadema na Ukawa, walifanya hivyo kwa kuona kuwa fursa ni kidogo, kwamba alikuwa na nafasi finyu ya kuishinda CCM na kushinda urais. Fursa za kisiasa huchochea mapenzi kwa wanasiasa, huyafifisha yaliyokuwepo, vilevile kuibua chuki palipokuwa na upendo.

NAZIDI KUKUMBUSHA

Wanasiasa hupendana kwa maslahi na huchukiana kwa maslahi. Siku zote uwe makini unapopendwa na mwanasiasa. Ukichukiwa na mwanasiasa ujue unaingilia maslahi yake.

Chukua hii; Katika siasa fursa huleta upendo, vilevile fursa huzalisha chuki.

Ndimi Luqman Maloto

Yusuph Manji Kuwaanika Maadui Wote wa Yanga

$
0
0

Klabu ya Yanga imetangaza ajenda kumi na moja kwa ajili ya mkutano mkuu wa dharura uliopangwa kufanyika Oktoba 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam.


Katika ajenda hizo, moja imeeleza kuwa katika hotuba yake, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, atawataja maadui wa klabu hiyo, huku kukiwa na msisitizo kuna mamluki wa wafanyabiashara wanaofanya mbinu za kuivuruga Yanga.


 Pamoja na ajenda nyingine 10, hiyo moja inaonekana kuanza kuwa gumzo kwenye mitandao, hasa kuhusiana na kwamba Manji atawataja maadui hao wa Yanga, ikielezwa wamepania kushusha hadhi ya klabu hiyo ili kuonyesha Manji ameshindwa.


“Kutakuwa na hotuba ya mwenyekiti, maoni na msimamo wake juu ya maazimio ya wanachama na kusema anayoyajua ya siri kuhusu Yanga na adui wa Yanga.


“Pia atafafanua wanaoleta vurugu, baadhi ni mamluki wa wafanyabiashara wenzake walioshindwa kumshinda kwa njia halali na sasa wanaitumia Yanga kama sehemu pekee iliyobaki kumuumiza kupitia mbinu zinazotumika.


 “Mbinu hizo ni kuleta vurugu ndani ya Yanga ili kumchafua binafsi ili kushusha hadhi ya klabu,” ilieleza sehemu ya jenda hiyo ya kumi na moja.


 Ajenda nyingine zilizotajwa ni pamoja na kupitia dondoo za kikao kilichopita, kuthibitisha wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, suala la kukodisha timu na nembo, kumjadili mwenyekiti (Manji) kuhusiana na kampuni inayotaka kukodisha ambayo ni yake na kubaki kwake katika uenyekiti. 


Itakuwa ni mgongano wa mawazo, kupitia utendaji wa kamati ya mashindano, kujadiliwa kwa wanachama ambao hawafiki kwenye vikao na wanakosoa kwenye vyombo vya habari tu na kujadili tarehe ya uchaguzi mdogo kujazia nafasi za wajumbe wa kamati ya utendaji.


Yanga iliamua kuitisha mkutano huo wa dharura baada ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza halitambui klabu hiyo kuikodisha timu yake na nembo yake kwa Kampuni ya Yanga Yetu Ltd.



Mkutano huo unasubiriwa kwa hamu, kwani hivi karibuni Manji alionekana kuudhika na kuendelea kusakamwa hadi kufikia kuona ajitoe Yanga. Lakini mwisho akabadili uamuzi na kusema, mkutano huo wa wanachama ndiyo utaamua juu yake kwa kuwa wanachama wengi wamekuwa wakimuunga mkono.


SOURCE: CHAMPIONI 

Trump: Kura zinaibiwa vituoni Marekani

$
0
0

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amedai uchaguzi nchini humo "unaibiwa" na vyombo vya habari pamoja na "kwenye vituo vya kupigia kura" kumzuia kushinda.

Matamshi hayo yanaonekana kukinzana na ya mgombea mwenza wake Mike Pence, ambaye awali aliambia kituo cha runinga cha NBC kwa Bw Trump bila shaka atakubali matokeo ya uchaguzi, licha ya "kuonewa" na vyombo vya habari.

Mshauri wa Bw Trump, Bw Rudy Giuliani pia amewatuhumu wanachama wa Democratic kwa "udanganyifu".

Kura za maoni zinaonesha kwamba Bw Trump anapoteza ushawishi katika majimbo mengi muhimu yanayoshindaniwa.

Hayo yakijiri, mgombea mwenza wa mpinzani wa Trump, mgombea wa chama cha Democratic Bi Hillary Clinton, Bw Tim Kaine amejibu vikali madai hayo ya Bw Trump kwamba kuna njama ya kuiba kura uchaguzini na kusema ni mbinu tu za kutaka kuzua wasiwasi.

Bw trump ametilia shaka uhalali wa shughuli ya sasa ya uchaguzi kwenye msururu wa ujumbe kwenye Twitter.

Ameandika hatimaye kwamba: "Uchaguzi huu bila shaka unaibiwa na wanahabari wasio wa kweli na wa kupotosha ambao wanamtetea Hillary mwovu - lakini pia katika vituo vingi vya kupigia kura - Inasikitisha."

Awali, Bw Trump alikuwa amewatuhumu wanahabari kwa kuchapisha habari za uongo.

"Uchaguzi huu unaibiwa na wanahabari, kwenye juhudi za pamoja wakishirikiana na wanakampeni wa Clinton, kwa kuchapisha habari za mambo ambayo hayajawahi kutokea!"

 Hata hivyo akiongea katika kipindi cha NBC cha Meet The Press (Kutana na Wanahabari), Bw Pence amesema Wamarekani wamechoshwa na mapendeleo ya wazi kwenye vyombo vya habari vya taifa ambapo kunaonekana dalili za "wizi wa uchaguzi".

Hata hivyo alisema: "Bila shaka, tutakubali matokeo ya uchaguzi."

"Uchaguzi daima huwa si rahisi," aliongeza, lakini akasema kwamba Marekani ina desturi ya "kukabidhi madaraka kwa njia ya amani


Hayo yakijiri, meya wa zamani wa New York Rudy Giuliani, ambaye ni mshauri wa kampeni wa Bw Trump aliambia kipindi cha State of the Union cha CNN kwamba ni "juha" peke yake anayeweza kuamini kwamba uchaguzi, mfano katika maeneo kama vile Philadelphia na Chicago, utakuwa wa haki.

"Nimepata visa vichache sana ambapo Republicans hutumia udanganyifu uchaguzini .... hawadhibiti maeneo ya ndani mitaani kama ilivyo kwa Democratic. Labda kama Republican wangedhibiti maeneo ya ndani mitaani, wangetumia udanganyifu kama wafanyavyo Democratic," alisema.
"Samahani. Wafu kawaida hupigia sana Democratic kuliko Republican" aliongeza.

Trump 'aliwapapasa wanawake kama pweza'

Mgombea mwenza wa Democratic Bw Kaine aliambia kipindi cha ABC cha This Week Mr Trump kwa sasa anatafuta kila "kivuli" na kuanza kukishambulia kwa sababu "anajua kwamba anashindwa".

"Anawalaumu wanahabari. Analaumu GOP (Chama cha Republican). Anasema Marekani haiwezi kuwa na uchaguzi huru na wa haki."

Wanawake kadha wamejitokeza na kumtuhumu Bw Trump kwa kuwadhalilisha kimapenzi kwa kuwapapasa au kuwapiga busu kwa lazima wiki iliyopita kwenye vyombo vya habari.

Hii ilijiri baada ya ukanda wa video wa mwaka 2005 kutolewa ukionyesha Bw Trump akitumia lugha ya kuudhi kuwarejelea wanawake.

Amekanusha madai hayo na kuwataja wanawake hao kama "waongo" na akawalaumu wanahabari akisema wamekuwa mawakala wa "mashine ya Clinton".

Waziri Mkuu Aagiza Mapato ya Hospitali ya Nachingwea Yakusanywe Kwa Njia ya Kielektroniki

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Bw. Bakari Mohammed kuhakikisha hospitali ya wilaya hiyo inakusanya mapato kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.


Ametoa agizo hilo jana Jumapili, Oktoba 16, 2016  wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Nachingwea akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Lindi.


Waziri Mkuu amesema Serikali ilishaagiza taasisi zote za umma kutumia mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma.


Amesema taasisi ambazo tayari ziameanza kutumia mfuko huo katika ukusanyaji wa mapato zimeweza kuongeza kiwango cha makusanyo kutoka sh. 300,000 hadi milioni nne kwa siku.


Pia aliwaagiza viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao utawawezesha kupata huduma ya matibabu bure katika kipindi cha mwaka mzima.


Akizungumzia kuhusu matibabu kwa wazee, Waziri Mkuu amemuagiza Bw. Mohammed kuhakikisha anafungua dirisha la kuwahudumia wazee ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma wanapofika hospitalini hapo.


“Mkurugenzi hakikisha watendaji wako wa kata na vijiji wamebaini wazee wote katika maeneo yao na kuwatengenezea vitambulisho vitakavyowawezesha kupatibiwa bure,” amesema.


Naye Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Samwel Laizer amesema muamko mdogo wa jamii kujiunga na CHF ni moja kati ya changamoto zinazowakabili katika utoaji wa huduma za afya.


Dk. Laizer amasema kati ya kaya 30,000 zilizoko wilayani Nachingwea ni kaya 7,133 tu ndizo zilizojiunga na mfuko wa CHF.


Awali Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa Chuo Cha Walimu na kuwataka wabadilike ili waweze kuwatumikia wananchi kwa uadilifu bila ya kujali itikadi zao za kidini na kisiasa.


Amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuwatumikia wananchi. “Serikali haitaridhika kuona wananchi wakizagaa kwenye ofisi za halmashauri hiyo bila ya kusikilizwa,” amesema.

Wakuu wa Wilaya 'Washindana' Kuwaweka ndani Wanasiasa

$
0
0
Wakuu wa wilaya mbalimbali nchini wameanza kuwasweka mahabusu baadhi ya watendaji na wanasiana ambao wanakwenda kinyume na maagizo yao ili kurejesha uwajibikaji katika maeneo yao.

Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997, kifungu cha 15 (1) inawapa mamlaka wakuu wa mikoa na wilaya kutoa amri ya mtu kukamatwa na kuwekwa ndani kwa saa 48 pale anapobaini kwamba mhusika ametenda kosa fulani.

Wakuu wa wilaya sasa wanatumia mamlaka hayo pale watendaji wao wanaposhindwa kutimiza maagizo yao. Suala la watendaji kuwekwa ndani limeshuhudiwa katika wilaya za Sengerema, Arumeru, Rorya na Newala.

Oktoba 13 mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alimsweka ndani kwa saa 12 kaimu mkurugenzi wa wilaya hiyo, Oscar Kapinga na kaimu mhasibu wa halmashauri hiyo, Paul Sweya kwa kushindwa kutekeleza agizo la mkuu huyo la kutafuta fedha kwa ajili ya kuwalipa wanaofanya usafi katika mji wa Sengerema.

Inaelezwa kuwa watu hao wanaofanya usafi hawajalipwa fedha zao kwa zaidi ya miezi sita, jambo lililomsukuma Kipole kuagiza walipwe.

Tukio jingine ni lile la Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti kuwaweka ndani madiwani wanne wa Chadema kwa madai kwamba wamekuwa wakimkwamisha kutekeleza kazi zake.

Miongoni mwa waliowekwa ndani ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Noah Lembrise ambaye alilala katika Kituo cha Polisi cha Usa River. Wengine ni Happy Gadiel, Nuru Ndosi na Winfrida Lukumay.

“Hawa (madiwani) wamekuwa wakivuruga ziara zangu kwa kupita kwa wananchi na kupotosha dhima ya Serikali kuhusu maendeleo.”

Huko Newala, Mkuu wa Wilaya, Aziza Mangosongo alimlaza katika Polisi kaimu meneja wa Mamlaka ya Maji Mradi wa Makondeko, Athumani Semkondo na fundi Mohamed Salum kwa saa 48 kwa kuvikosesha maji vijiji 14 vyenye wakazi 60,000.

Mangosongo alisema kulifanyika hujuma ya kuziba bomba ili maji yasipatikane katika vijiji hivyo lakini kaimu mkurugenzi huyo alishindwa kufuatilia taarifa aliyopewa kwamba vijiji hivyo havipati maji ili achukue hatua.

“Kama mkurugenzi alikuwa na taarifa na hakuchukua hatua, kuna nini kimejificha hapo? Lazima nitahisi kuna jambo ndiyo maana nikaamua akalale rumande kwa saa 48 kwa sababu nina mamlaka kisheria. Akae humo ndani kwanza ajitafakari,” alisema Mangosongo.

Hali kama hiyo ilitokea pia katika Wilaya ya Rorya baada ya mkuu wa wilaya hiyo, Simon Chacha kuwaweka ndani watu 10 akiwamo Diwani wa Kigunga (Chadema), Vitalis Joseph baada ya kutokea mgogoro kati ya vijiji viwili na kusababisha mazao kufyekwa.

Diwani huyo alifika eneo la tukio na kukuta mazao yamefyekwa, hata hivyo, Chacha aliagiza akamatwe na kuwekwa ndani pamoja na watu wengine kwa kuhusishwa na uharibifu huo.

“Tumewachukua baadhi ya watu ili kuisaidia Serikali kupata uhalisia wa tukio hili, na ninawaambia wananchi wa Rorya kuwa Serikali hii ya awamu ya tano haitaki mzaha na yeyote anayejitokeza kufanya vitendo viovu tutamshughulikia,” alisema Chacha.



Maoni ya wadau

Wadau mbalimbali wamepinga hatua ya wakuu wa wilaya kuwaweka ndani watendaji wa halmashauri wakisema wanafanya hivyo kwa lengo la kuwakomoa.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala amesema amri hizo zimekuwa zikitolewa katika maeneo ambayo upinzani unaongoza, jambo analolitafsiri kama ni kuwakomoa wapinzani.

Alisema sheria hiyo inatumika kukandamiza demokrasia kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake. Alisema wakuu wa wilaya wanatakiwa kutumia sheria inayowapa mamlaka hayo kwa wahalifu wa makosa ya jinai na wahujumu uchumi.

“Madiwani na wakurugenzi ni watendaji tu, kuwaweka ndani kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya mkuu wa wilaya ni kuwaonea. Sheria hiyo ya saa 48 itumike kwa wahalifu na wanaohujumu uchumi,” alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema sheria inayotumika bado ina sura ya kikoloni kwa sababu haiendani na taratibu za menejimenti ya watumishi.

Alisema kumweka mtumishi ndani siyo njia nzuri ya kumwajibisha kwa sababu uongozi wa sasa unafuata mfumo wa kufanya kazi kwa pamoja.

“Unapomweka mtu ndani tayari umemhukumu na mara nyingi amri hiyo inatolewa na wakuu wa wilaya ili kuonyesha kwamba wana uwezo wa kufanya jambo,” alisema.

Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi alisema wakuu hao wanataka kujijengea sifa kwa Rais wakidhani kwamba kuwaweka watu ndani ndiyo uwajibikaji.

Joseph Mungai Aibuka na Kusema "Kikwete Alinitosa ili Kuwafurahisha Walimu"

$
0
0
Joseph Mungai, ambaye alikuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni wa Serikali ya Awamu ya Tatu, amepinga vikali shutuma kuwa alishusha kiwango cha elimu, badala yake akairushia lawama awamu iliyofuata kuwa ilifanya maamuzi yaliyozorotesha sekta hiyo.

Mungai, ambaye alikuwa ajibu tuhuma zilizoelekezwa kwake baada ya kustaafu siasa, amesema hata kiongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete hakutaka kumteua kuendelea kuongoza elimu kwa kuwa alitaka kufurahisha walimu waliokuwa wakimchukia kutokana na kuwabana.

Mwanasiasa huyo mstaafu pia alipinga shutuma dhidi yake kuwa alifuta michezo shuleni, akisema hahusiki na suala hilo na alichokifanya ni kufuta michango ya mashindano ya Umiseta na Umitashumta na kutoa maelekezo michezo ifanyike nje ya muda wa masomo au mwishoni mwa wiki.

Mungai aliamua kuweka bayana masuala hayo wakati alipofanya mahojiano na mwandishi Luqman Maloto kuhusu mabadiliko makubwa ya elimu ambayo Serikali ya Awamu ya Tatu iliyafanya, lakini akaelekezewa lawama kuwa ndiye aliyeyafanya bila kushirikisha wadau na kusababisha kuanguka kwa elimu.

“Kama nilivyosema, nilijisikia vibaya kuona kazi nzuri tuliyoifanya chini ya uongozi wa Rais (Benjamin) Mkapa inabomolewa katika mwaka wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne,” alisema Mungai alipoulizwa alijisikiaje wakati anaona Baraza la Mawaziri linabadilisha uamuzi ambao waliufanya wakati akiwa Waziri wa Elimu.

“Nilisononeka sana. Pamoja na utu uzima wangu, sikusikilizwa. Niliwatahadharisha wahusika kuwa matokeo mabaya ya uamuzi huo watayaona baada ya miaka kadhaa. Matokeo yakawa kama nilivyosema. Baada ya mwaka 2007, matokeo ya mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne yalianza kushuka mwaka hadi mwaka.”

Mungai alisema katika kipindi hicho idadi ya wahitimu wanaofeli iliongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia kiwango cha juu mwaka 2012 wakati idadi ya waliofeli ilipofikia asilimia 60.

Alisema hata vyuo vikuu viliendelea na vinaendelea hadi sasa kupokea wanafunzi wasiojua vizuri Kiingereza kutokana na kufuta hata somo walilolianzisha la muundo wa Kiingereza kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu ya sekondari ili kuwaandaa na masomo ya chuo kikuu.

Mungai hakutaka kumlaumu mtu yeyote aliyeshika wizara hiyo, akisema katika kipindi cha miaka 55, takriban mawaziri 23 wameiongoza, ikiwa ni wastani wa miaka miwili kwa kila waziri na hivyo hakuna aliyepata muda wa kutosha.

Akizungumzia uamuzi ambao uongozi wake ulifanya wakati huo, Mungai alisema ni kubuni na kuanzisha Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) mwaka 2004 - 2009 uliopanua elimu ya sekondari kuwafikia angalau nusu ya rika lengwa la miaka 14-18.

“Tulianzisha vyuo vikuu vishiriki vya elimu vya Chang’ombe na Mkwawa kwa lengo la kufundisha walimu kwa ajili ya utekelezaji wa MMES. Upanuaji wa elimu ya sekondari ulipangwa kuendana na upanuaji wa mafunzo ya walimu wa sekondari,” alisema.

“Najivunia kufuta ada na kuifanya elimu ya msingi kuwa ya bila malipo na ya lazima kwa kila mtoto wa miaka saba hadi 13. Mzazi alibakia na wajibu wa kumpa mtoto wake malazi, mlo na mavazi. Nilipiga marufuku michango yote ya wanafunzi na wazazi wao. Michango ya ujenzi wa shule ni jukumu la wote wenye uwezo wa kufanya kazi; na siyo wazazi wa wanafunzi peke yao.”

Alisema wakati huo Serikali ilitoa ruzuku ya uendeshaji wa shule za msingi ya Sh10,000 kwa kila mwanafunzi, kutenga fedha kwa ajili ya michezo baada ya kufuta mchango wa Sh1,000 kwa ajili mashindano ya shule.

Mbali ya MMES, pia aliandaa na kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM) 2002 - 2006 iliyotoa ruzuku za maendeleo na uendeshaji kwa wananchi wanaojenga na kuendesha shule. Kadhalika, alisimamia kupunguzwa kwa ada ya shule za sekondari za Serikali za kutwa kwa aslimia 50 kutoka Sh40,000 mpaka Sh20,000 na kuongeza ruzuku maradufu ya kuwasomesha sekondari bila ada, watoto wa familia zisizo na uwezo.

Alisema anajivunia pia kuanzisha mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), katika vyuo vyote vya ualimu, kusimamia marekebisho na kuanza kutekeleza mtalaa mpya wa sekondari uliounganisha masomo ya michepuo (ufundi, kilimo, biashara na sayansi kimu) na masomo ya kawaida uliotokana na mapendekezo ya Taarifa ya Mfumo wa Elimu ya Tanzania unaofaa kwa Karne ya 21 (The Tanzania Education System for the 21st Century).

Alipoulizwa kitu ambacho angetamani kuendelea kukisimamia wakati Serikali ya Awamu ya Nne ikiingia madarakani, Mungai alitaja maboresho ya elimu kwa kutekeleza mtalaa mpya.

“Lakini Rais Kikwete aliniteua kuwa Waziri wa Kilimo na baadaye kidogo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Niligundua baadaye kuwa lilikuwapo shinikizo la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) nisiteuliwe kuwa Waziri wa Elimu. Sikupendwa na walimu kwa sababu niliwabana mno,” alisema.

“Wakajibu mapigo kwa kumwambia mgombea urais wa CCM mwaka 2005 (Kikwete) kuwa wanamuunga mkono, lakini Mungai asiwe tena Waziri wa Elimu. Rais Kikwete akaamua kuwafurahisha zaidi walimu kwa kumteua aliyekuwaRrais wa Chama cha Walimu, Mheshimiwa Margareth Sitta kuwa Waziri wa Elimu baada yangu. Hivyo ndivyo siasa ilivyo.”

Mkurugenzi Mbaroni Kwa Kujifanya Usalama wa Taifa, na Kutishia kwa Bastola

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro baada ya kujifanya Usalama wa Taifa nakumtishia kwa Bastola askari wa usalama barabarani wakati wakielekea kituo kidogo cha polisi kingoluwira, alikotaka apelekwe kuzungumza na mkuu wa kituo baada ya kukamatwa akiwa amezidisha mwendo kasi (Speed)
 Tukio hilo limetokea barabara kuu ya Morogoro - Dar es salaam

Chanzo :ITV

Lowassa na Jakaya Kikwete Uso Kwa Uso..

$
0
0

Hatimae leo Msiba wa Masaburi umewakutanisha Lowassa na Kikwete. Kinyume na matarajio ya Wengi kwamba wawili hawa hawaongei kutokana na bifu zao za kisiasa lakini walipo kutana wamekumbatiana wamecheka kwa bashasha sana bila shaka kesho magazeti mengi yatauza picha yao.
Viewing all 2111 articles
Browse latest View live