Quantcast
Channel: Siasa Huru
Viewing all 2111 articles
Browse latest View live

Jinsi ya Kujua Kama Simu Yako Imeingiliwa na Mtu Anakuchunguza Kwa Siri

$
0
0
Kama una hofu kuwa kuna mtu anakufuatilia kwa siri au anakuchunguza (spying) kwenye simu yako, hauko mwenyewe. Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na idadi kuwa ya watu wakilalamika kuwa wamekuwa wakifuatiliwa katika simu zao bila ridhaa yao na bila wao kujua.

Lakini kwa upande mwingine ni kuwa, kuna jinsi unaweza kufanya au ishara ambazo ukiziona zinakuonyesha moja kwa moja kuwa simu yako imeingiliwa na kuwa kuna mtu anakuchnguza kwa siri.

Kufahamu viashiria hivyo, twende wote hadi mwisho wa makala hii.

1. Kama betri ya simu yako inaisha chaji haraka kuliko kawaida, chunguza huenda kuna programu inayojiendesha bila ya wewe kujua.


Kama kwenye simu yako hauna ‘games’ nyingi ambazo ukicheza mara kwa mara zinasababisha betri ya simu yako kuisha haraka, basi huenda sababu ni programu inayochunguza simu yako. Wakati mwingine simu huchukua muda mrefu kuchaji, hii ni kutokana na sababu kuwa wakati wewe umeweka simu chini unachaji, programu inayokuchunguza kwenye simu yako, inafanya kazi.

2. Kama simu yako huwa ya moto wakati wote.

Simu mara nyingi hupata moto inapokuwa inatumika, sasa kama simu yako umeiweka tu mfukoni au mezani lakini ukija unakuta ina moto kiasi kwamba unaweza kuchemsha yai, kutakuwa na programu zinazojiendesha kwenye simu yako. Kupata joto huku hakuhusiani na wakati wa kuchaji sababu simu nyingine hupata moto wakati zinachajiwa.

3. Kama wakati unaongea na simu unasikia kelele za ajabu au mwangwi hata kama unayeongea naye yupo sehemu tulivu.

Kama hali hii haikuwapo awali, yaani kama ulikuwa unaongea na simu kawaida lakini ghafla ukiongea unasikia kelele za ajabu na mwangi, huenda simu yako ina programu zinazojiendesha ndani ambazo hutumika kukuchaunguza wewe kwenye simu yako.

Kama utaona dalili moja kati ya hizo kwenye simu yako, unaweza kupakua ‘Anti-spyware applications’ ambazo zitakuwasaidia kuilinda simu yako pasiwepo na programu zinazojiendesha zenyewe bila ridhaa yako na zikatumika kukuchunguza.

JINSI YA KUJUA KAMA SIMU YAKO IMEINGILIWA NA MTU ANAKUCHUNGUZA (SPY) KWA SIRI

Hawa Ndio Wanasiasa 10 wa Tanzania Wenye Uwezo wa Kutoa Hotuba za Kusisimua

$
0
0
Katika kufuatilia uwezo wa kujenga hoja, kuwasilisha mada kwa walengwa kulingana na makundi yao na uwezo wa kuvuta hisia za wasikilizaji, hawa ndio wanasiasa kumi wanaonivutia zaidi ktk hotuba zao(kwa fikra zangu huru)?

1. Aman Abedi Karume
2. Godbless Lema
3. Tundu Antipas Lissu
4. Yusuph Makamba
5. Christopher Ole Sendeka
6. Freeman Mbowe
7. Cosato Chumi
8. James Mbatia
9. Felix Mrema
10. Zitto Zubeir Kabwe

Wabunge Walio Wengi Hawasikiki...Nini Kimewasibu?

$
0
0
Nimefuatilia kwa karibu katika media mbalimbali,na kugundua yafuatayo.
Wabunge wengi hawasikiki ktk media mbalimbali wakihamasisha masuala ya maendeleo ktk majimbo yao. Huko nyuma ilikuwa tofauti. Kwa tahmini yangu ya karibu,nahisi wameanza kuridhika na kasi ya utendaji wa Serikali na hivyo wao kuwa na kazi kidogo ya kufanya

Lowassa, Lipumba na Slaa waunde Chama Kimoja!

$
0
0
Kuna kila dalili kua ukaaji wa Lowasa Chadema sio wa kudumu, unategemea tu kama some factors na kama hazitakuwepo, definitely ataondoka!

Lipumba naye nia yake ya kuendelea kusikilia hapo buguruni, unaweza kukatizwa muda wowote! Kama baadhi ya mambo hayatakwenda sawa!

Slaa naye, baada ya kupumzika vya kutosha huko Canada, nadhani ameshakusanya materials ya kutosha kurudi kwa spidi yake ya awali, hii ni baada ya kuoneshwa mlango wa kutokea pale chadema baada ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo!

Wanasiasa hawa watatu wanafanana sana katika mambo haya;

1. Wanauzoefu wa kutosha wa siasa za Tanzania.

2. Wana wafuasi ambao wapo tayari kwenda walipo " ulipo tupo"

3. Hawana furaha au uhakika wa usalama wa maisha yao ya kisiasa, hapo walipo sasa.

4. Ni wa pambanaji.

Factors hizi zinawafanya kutengeneza bond , ama combination nzuri , kwa wale mashabiki wa mpira unaweza ifananisha na kikosi cha ushambuliaji cha timu ya Barcelona!

Siasa ndivyo ilivyo!

Kila Nipatapo Nafasi Kazi Yangu ni Kufunga-Kichuya

$
0
0
Mshambuliaji wa timu ya Simba anayeongoza kwa kufunga magoli 7 katika mechi 9 alizocheza ligi kuu Tanzania bara msimu huu Shiza Kichuya amesema kila atakapo pata nafasi kazi yake ni kufunga.

Kichuya ameyasema hayo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam baada ya kumalizika kwa mchezso kati ya Simba na Kagera Sugar mtanange ambao umemalizika kwa Simba kuibuka kidedea kwa kuicharaza Kagera Sugara bakoran 2 kwa bila.

“Wachezaji kazi yetu ni kufunga, na mimi kila nitakapopata nafasi kazi ni kufunga na lengo letu ni kuendelea kuwa wamoja kama ilivyo sasa ambapo mashabiki pamoja na viongozi na wachezaji tupo wamoja ndiyo maana hata matokeo yanaonekana” Amesema Kichuya

Wakati huo huo Nahodha wa Kagera Sugar George Kavila amesema Simba imepata nafasi na kuzitumia vizuri ndiyo maana wakaweza kuibuka na ushindi huo

“Ligi hii ni ngumu huwezi kusema wameshinda kwa bahati, wamepata nafasi wakazitumia tutaenda kujipanga vizuri kwa michezo inayofuata” Amesema Kavila

Uchumi Wanyauka..Bank Kuu Wakiri Hali ni Mbaya..Gazeti Jambo leo Laandika

$
0
0
Uchumi Wanyauka..Bank Kuu Wakiri Hali ni Mbaya Mzunguko wa fedha na utoaji mikopo sekta binafsi

AT: Nimechoka Kutambulishwa Msanii wa Zanzibar, Mimi ni Msanii wa Tanzania

$
0
0
AT amesema inatosha sasa watu kumchukulia kama msanii wa Zanzibar. Anataka atambulike kama msanii wa Tanzania, vile vile Diamond au Alikiba hutambulishwa.

Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, AT amewakumbusha mashabiki na wadau wa muziki kuwa hakuna tofauti kati ya msanii anayetokea Njombe, Sumbawanga na Zanzibar kwakuwa wote ni Watanzania. Amedai kuwa wote hao wanatoka mikoa tofauti lakini taifa moja.

Amemtolea mfano Baby J kuwa ni msanii aliyeishi Zanzibar lakini asili yake ni Usukumani na kwamba alienda huko na kuanzia darasa la saba lakini wanajivunia kuwa ni ndugu yao.

“Lakini kwa upande wa bara mpaka leo AT akifanya show anaambiwa kutoka Zanzibar. Lakini wakipanda Weusi ‘aah bwana wanakuja Weusi.’ Hii nayo inaleta matabaka. Huwezi kusema huyu anatoka Zanzibar, huyu hapa anatoka Mwanza, show inafanyika Sumbawanga au inafanyika Njombe. Ni sawa sawa na kusema kuna abiria 10 na mmasai mmoja,” amesisitiza.

Ameeleza kuwa hata suala la tuzo akishinda yeye, watu wataishia kusema ameiapa sifa Zanzibar na si Tanzania.

“Alikiba kwao Kigoma, kwahiyo akishinda tuzo tuseme tuzo kawapa Kigoma,si ni tuzo ya Mtanzania?” amehoji.

Hatukuomba kuja Bariadi, hatuna uwezo wa kurudisha fedha za Mwenge – Madereva

$
0
0
Madereva na wasidizi wa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mbalimbali waolikuwa tayari wameshafika mkoani Simiyu kwaajili ya kusherehekea kilele cha mbio za mwenge, wameeleza kuumizwa na agizo la Rais John Magufuli la kurejesha fedha za kujikimu.

Baadhi wamesema kuwa hawana uwezo wa kuzirejesha fedha hizo kwani hawakuwaomba kufanya safari hizo kwwakuwa ilikuwa sehemu ya kazi zao kwahiyo kiasi cha fedha hizo walizitumia kama walivyokubaliwa na ofisi kuwawezesha na kufika katika eneo hilo.

“Sisi hatukuomba kuja Bariadi kwenye sherehe za mbio za Mwenge wa uhuru, tuliambiwa kuja na tukapewa fedha ambazo tumezitumia kwa mujibu wa mahesabu ya matumizi tuliyoandikiwa kwasababu ilibidi tule na kulala kwenye nyumba za wageni,tutapata wapi hela za kuzirudisha, hapo sisi kosa letu liko wapi,”? alihoji mmoja wa madereva aliliambia gazeti la The Citizen.

“Ili nibidi nilipe chumba kwa siku 7 ambazo nilitarajia kuishi hapa kama nilivyotumwa kwa uhaba wa vyumba,sasa naanzaje kumwambia mmenyewe arudishe fedha yote ili niirejeshe ofisini ?alihoji.

Wiki iliyopita Rais John Magufuli alisitisha safari ya viongozi wa mikoa na wilaya kwenda Simiyu kwenye kilele cha mbio za Mwenge na kuwataka wale waliokwisha chukua posho kuzirejesha.

Sakata la Escrow Lilivyosababisha Mapigo Mawili Kwa Mpigo Kwa Serikali

$
0
0
ILIANZIA kwa David Kafulila, mwanasiasa kijana aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, aliposema ndani ya bunge mgogoro uliohusu uchotwaji wa fedha kifisadi zilizokuwa Akaunti ya Tegeta Escrow, umeikosesha nchi mamilioni ya shilingi kutoka Marekani, anaandika Bariki Masudi.
Kafulila alisema serikali ya Marekani kupitia shirika lake la Mfuko wa Misaada wa Milenia (MCC) imekataa kuidhinisha msaada wa zaidi ya Dola 470 milioni kwa Tanzania kutokana na ufisadi huo.

Harakaharaka akaibuka Saada Mkuya Salum, aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi chini ya serikali ya Dk. Jakaya Kikwete, akakana na kumsema Kafulila kuwa anapotosha bunge.
Ikumbukwe wakati huo, tayari Kafulila alishagombana na wakubwa wa serikali hasahasa Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini na Jaji Fredrick Werema aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, ambaye alimuita mbunge huyo “tumbili.”

Prof. Muhongo na Jaji Werema walikuwa midomoni mwa wabunge wa upinzani kwa kutuhumiwa kuridhia ufisadi wa fedha za Escrow, baada ya kuruhusu zitolewe kwenye akaunti iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kusubiri kumalizika kwa mvutano wa Shirika la Umeme (TANESCO) na Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Waziri Saada akilalamika na kumtaka Kafulila afute kauli yake, alisema bungeni, “Si kweli mheshimiwa Spika. Fedha za MCC zitapatikana tukishakamilisha mambo madogo tu yaliyobaki. Hakuna tatizo na fedha hizi, mbunge asipotoshe bunge.”

Kafulila alikataa shinikizo la kufuta kauli, na akashikilia alichokisema.
Ukapita mwezi, miezi na baadaye ikatoka ripoti ya Bodi ya MCC, iliyopitishiwa ofisi ya ubalozi wa Marekani nchini, ikisema msaada umesitishwa mpaka wakati mwingine baada ya masharti kadhaa kutekelezwa, likiwemo la serikali kueleza kwa uwazi fedha zilivyotoka.

Matumaini ya serikali yakaanza kufutika ilipoelezwa na MCC kuwa Bodi imekataa kwa mara nyingine kuidhinisha kutolewa kwa msaada kwa Tanzania. Dhahiri sasa matumaini hayapo tena, maana Bodi ya MCC imeshafunga ofisi zake nchini.

Uamuzi huu mpya umekuja wiki moja baada ya Mahakama ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara iliyoko London, Uingereza kuipa ushindi Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) katika kesi iliyofungua dhidi ya Tanesco, ikidai uhalali wa kumiliki mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL iliyoko Tegeta.

Benki ya Standard Chartered (SCBHK) imeshinda kesi na kuamuliwa ilipwe mamilioni ya dola na kuhalalika kuwa mmiliki wa mitambo hiyo kwani haijalipwa deni lililotokana na kukopesha IPTL fedha zilizotumika kuinunulia.

Mapigo mawili kwa mpigo dhidi ya serikali – kwanza kunyimwa kabisa msaada wa mamilioni ya dola, na pili kulipishwa mamilioni mengine kama adhabu dhidi ya Tanesco iliyoshindwa kesi mahakamani.

Yote haya mawili na athari zake kubwa kwa maendeleo ya nchi, yametokana na ukaidi, uzembe, ubazazi na ujinga wa serikali wenyewe. Iliambiwa haikusikia, iliposikia haikuzingatia, haikuchukua hatua zilizofaa, ikaridhia baadhi ya wakubwa kunufaika kifisadi.

Desturi haitabadilika: Kweli hubakia kweli (haifutiki) na uongo hujitenga. Havitengamani. Niseme haki hubaki haki, kamwe haishikani na batili. Shida ni pale wa serikali ya CCM wasipojifunza.

Vita Kuu ya Tatu ya Dunia, Rais wa Urusi Putin Aagiza Watu Wote wa Urusi Wanaoishi Nje Warudi Nyumbani

$
0
0
Kiongozi wa taifa kubwa na tajiri duniani mh Putini wa urusi hapo jana ametoa amri kwa raia wake waishio nje ya urusi kurudi haraka iwezekanavyo katika ardhi ya nyumbani,

Kutokana na mgogoro unaoendelea katika ardhi ya syria na kupelekea mkanganyiko wa kidiplomasia juu ya mataifa ya magharibi kuhusu mapigano yanayoendelea kati ya serikali na makundi ya waasi.

Hatua hiyo imefikia kwa taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali kufikia kwa bw Putini kuwaagiza watumishi wote wa serikali na maafisa wa kijeshi wenye watoto wanaosoma nje ya urusi kurudi haraka iwezekanavyo la sivyo hawatoajiriwa na serikali yao pale watakapo kaidi amri hiyo.


Tazama Video:

Assist ya Samatta Imeinusuru KRC Genk na Kipigo Cha Tano Msimu Huu

$
0
0
Baada ya watanzania kupokea good news ya nahodha wao wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta kuteuliwa katika list ya majina 30 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika 2016, nyota huyo usiku wa October 15 alishuka dimbani kuisaidia timu yake ya KRC Genk kuwania point tatu ugenini dhidi ya Mouscron.

Samatta ambaye alianzia benchi na kuingia kipindi cha pili dakika ya 67 kuchukua nafasi ya mjamaica Leon Bailey, alishuhudia timu yake ya KRC Genk ikiwa nyuma kwa goli 2-1 hadi alipoingia kwenda kuongeza nguvu dakika ya 78 akafanikiwa kutoa assist na kuinusuru KRC Genk isipoteze mchezo wa tano wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu huu.

Kufuatia matokeo hayo KRC Genk inakuwa nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji, magoli ya KRC Genk yote yalifingwa na mgiriki Nikolaos Karelis dakika ya 33 baada ya kutumia vyema pasi ya Pozuelo na 78, wakati magoli ya Mouscron yalifungwa Hassan Mahmoud dakika ya 3 na Valentin Viola dakika ya 42.

Diamond, Harmonize na DJ D-Ommy Washinda Tuzo za Afrimma 2016

$
0
0
Diamond Platnumz, Harmonize na DJ D-Ommy, wameibuka washindi kwenye tuzo za Afrimma 2016, zilizofanyika Dallas, nchini Marekani Jumamosi hii.

Diamond ameibuka tuzo ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki, Harmonize Msanii bora chipukizi na D- Ommy, DJ bora wa Afrika.

“Team Tanzania Mungu ni mwema siku zote,” ameandika Harmonize baada ya ushindi huo.


Issue ya Mikopo ya Elimu ya Juu itamharibia sana JPM

$
0
0
Vyuo vya elimu ya juu vimefunguliwa huku wanafunzi wengi wakiwa njiapanda kuhusu mikopo yao ya ada pamoja na chakula na malazi. Suala la means testing kwa mwaka huu limekuwa tight sana kiasi kwamba kuna wanaojuta kuomba kudahiliwa na vyuo kwa sababu hata ule mkopo wa chakula na malazi hawapewi wengi wao na huwezi kusajiliwa chuoni bila kulipa angalau ada ya semester moja!

Serikali inasema inaweka kipaombele kwa baadhi ya kozi/fani,fine bt ni asilimia ndogo saaana ya wanafunzi wanaochukua fani hizo za kipaombele ukilinganishwa na wengine,haiwezekani wooote wasome Petroleum Engineering,architechture,medicine,anatomy, and the like!

Na wengi wa watoto wa maskini ndo hawa waliosomea shule za Kayumba ambako Physics na Biology ni msamiati mgumu sana so walilazimika kusoma masomo ya arts ili waweze kufaulu kwa sababu ya kukosa walimu wa sayansi na miundombinu ya maabara.

Nionavyo mm,pesa nyingi inatumika zaidi huku kwenye 'ELIMU BURE',hali ikiwa mbaya zaidi hawa wanafunzi wa elimu ya juu wanaweza kugoma na hii itamletea shida kubwa sana JPM. Naomba washauri wake mliopo humu #JF mumfikishie salamu hizi,watoto wengi wa maskini ndo waliosoma masomo ya arts na ndo wanaokosa mikopo.

Siku 158 za Mabasi ya Mwendo Kasi...Hali ni Tete Yaamua Kupunguza Wafanyakazi

$
0
0
Wakati Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi Dar es Salaam (Dart) ukiwa umefikisha siku 158 tangu ulipozinduliwa Mei 10, kampuni inayouendesha imelazimika kupunguza wafanyakazi kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa.

Nauli za mabasi hayo yaliyolenga kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, zilitangazwa Mei 9, ikiwa ni siku moja kabla ya uzinduzi wa safari zake.

Nauli hizo zilizotangazwa na mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Johansen Kahatano ni Sh800 kutoka Mbezi Mwisho hadi Kivukoni na wanafunzi ni Sh200.

Nauli kutoka Mbezi Mwisho-Kimara hadi Kariakoo Sh800 na Kutoka Morocco - Kimara hadi Mbezi Mwisho ni Sh800 na kutoka Morocco - Kivukoni Sh650, sawa na Kariakoo hadi Morocco.

Lakini nauli hizo zinazonekana kutokidhi gharama za uendeshaji.  Katika kutathmini siku 158 tangu kuanza kwa huduma hiyo, Mwananchi ilizungumza na David Mgwassa, mkurugenzi mtendaji wa Udart inayoendesha mradi huo ambaye alisema gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko mapato.

“Kwa siku tunapakia abiria 120,000, lakini gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko mapato kwa sababu nauli tuliyopewa ni chini ya ile tuliyoomba na iliyowekwa kwenye mkataba,” alisema Mgwasa.

Wadau Waanza Kuhoji Elimu ya Mbowe..Wadai Aonyeshe Cheti Chake cha Form Four

$
0
0
By Lizaboni
Nianze kwa kusema kuwa lengo la chama chochote cha siasa ni kutwaa dola. Chama cha siasa si kama chama cha Mpira wa miguu ama chama cha kuimba muziki wa singeli. Kwa maana nyingine chama kinachoshinda uchaguzi ndicho hutwaa mamlaka ya nchi na ndicho huunda Serikali. Ni kwa muktadha huo, Kiongozi wa Chama cha Siasa anapaswa kuwa na sifa zile zile ambazo kiongozi wa nchi anapaswa kuwa nazo. Hata kama Mwenyekiti wa chama kilichoshinda hajagombea, ataendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho na atasimamia utendaji wa Rais wake.

Hii ni hoja ya msingi sana na sijajua kwa nini wasomi wengi bungeni akina Tundu Lissu hawalioni? Sijajua pia kwa nini washirika wa ukawa akina James Mbatia hawalizungumzi kwa lengo la kutoa hoja ili lijadiliwe bungeni.

Wadau, chaka kikiongozwa na kihiyo madhara yake ni makubwa. Chama kinakuwa cha hovyo na kinakuwa na watu wa hovyo. Ndo maana hata kwenye uchaguzi wanafanya hovyo. Kwani Mwenyekiti hovyo huzaa chama hovyo na wafuasi hovyo.

Tuache masihara katika masuala ya nchi. Hivi mliwahi kujiuliza kwa sasa kwa nini Mbowe hana hamu ya kugombea Urais? Anatamani sana tena sana ila vigezo na masharti havikidhi. Ni Form Four Leaver! Nasikia hata hicho cheti cha form four alikipata kimagumashi. Ndio maana humsikii anasema lolote kuhusu vyeti feki kwa vile hata yeye ana cheti feki cha kidato cha Nne.

Taarifa zilizopo ni kwamba, Freeman Mbowe hakuwahi kufanya na kufaulu mtihani wa Kidato Cha Nne lakini ana cheti cha Form Four. Hakuna ushahidi na wala uthibitisho kuwa alifanya mtihani huo. Je Mbowe alipataje cheti cha Form Four wakati hajawahi kufanya na kufaulu mtihani huo? Nini kilichopo nyuma ya pazia? Nani alisimamia hilo?

My brother Freeman Aikael Mbowe, ili kuondoa shaka hiyo kuwa hujafanya na kufaulu mtihani wa kidato cha Nne, hebu jitokeze hapa au wape wale vijana wako waiweke hapa kuondoa huo utata. Kuendelea kukaa kimya ni sawa na kuhalalisha kuwa kisemwacho kipo.

Katika kurahisisha utetezi wako, hebu jibu maswali haya.

1. Je ulianza kidato cha kwanza mwaka gani na ulimaliza lini?
2. Ulisoma shule gani?
3. Wakati unamaliza kidato cha Nne, Mkuu wako wa Shule alikuwa anaitwa nani?
4. Unakumbuka namba yako ya usajili wa mtihani wa Form Four? Itaje.
5. Matokeo ya Form Four yalikuwaje? Je yalikuwezesha kuendelea na elimu ya kidato cha Tano?
6. Ambatanisha vielelezo ikiwa ni pamoja na nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne

By Lizaboni/Jamii Forums


Kamati ya Mufti yashtukia Ulaji Mali za Bakwata, ‘Yapiga Pini’

$
0
0
Kamati ya Bakwata iliyoundwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir kufuatilia mali za baraza hilo imepiga marufuku kuuzwa na kupangisha hadi itakapomaliza uchunguzi wake.

Agosti 9, mwaka huu, Sheikh Zubeir aliunda kamati ya wajumbe nane kwa ajili ya kushughulikia masuala mbalimbali, ikiwamo misamaha ya kodi iliyoombwa na Bakwata na taasisi zake.

Kamati hiyo inaongozwa na Sheikh Abuubakar Khalid akiwa mwenyekiti, Sheikh Issa Athman Issa (Makamu) na Mwalimu Ahmed Abeid (Katibu).

Waraka uliotolewa jana na kamati hiyo kwenda kwa masheikh wa mikoa na wilaya ulieleza kwamba kiongozi yeyote wa Bakwata haruhusiwi kuingia mkataba wa kuuza na kupangisha nyumba za baraza hilo.

Pia, kamati ilipiga marufuku kuhamisha mali yeyote au kuingia ubia na mwekezaji au kuingia mikataba mipya, hadi pale kamati hiyo itakapomaliza kazi yake.

Waraka huo ulisisitiza kuwa agizo hilo ni halali kwa mujibu wa Katiba ya Bakwata na linapaswa kufanyiwa kazi ipasavyo.

Maalim Seif 'Kinachoendelea ni Mpango Ulioandaliwa wa Kuvuruga CUF'

$
0
0

Mwanasiasa Maalim Seif azungumzia mgogoro wa Chama cha CUF. Asema kinachoendelea ni mpango ulioandaliwa wa kuvuruga jitihada za chama hicho kudai haki Zanzibar “Nasema hiyo ya Profesa Lipumba ni ajenda iliyolenga kutuparaganya ili tuondoke katika mazingira na hima ya kutetea haki yetu iliyoporwa. Lakini msijali hiyo haitafanikiwa nasi tumefikia pazuri sasa,” alisema Seif

Alilaumu juhudi alizoziita za baadhi ya watu kutumia vibaya mamlaka kutaka kumzuia asiongee na wananchi licha ya kuwa umma unayo shauku kubwa ya kuhitaji kumsikiliza kila anapopita. “Najua zipo kila mbinu na hila za kutaka mimi nisiongee nanyi. Wenyewe mmeshuhudia hapa msikitini baada ya kubainika nakuja, lakini nasema mimi ni binadamu na kiongozi, ninayo haki ya kuongea na yeyote popote.Nitaongea na nitaongea popote pale,” alisema.

Nyayo 400 za Binadamu wa Kale Zangunduliwa Bonde la Ol Doinyo Lengai

$
0
0

Wanasayansi wagundua nyayo 400 za binadamu wa kale katika tabaka la ardhi linalokadiriwa kuwa na miaka 19,000 eneo la Ol Doinyo Lengai, Arusha.

Nyayo hizo ni za makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wametembea juu ya tope la majivu ya volcano pembezoni mwa Ziwa Natron katika eneo lililopewa jina la Engare Sero sio mbali na mlima wa volcano wa Ol Doinyo Lengai (Mlima wa Mungu kwa tafsiri ya Kimasai).

Sababu Muhimu Kwanini Urusi Hawezi Shinda Vita Dhidi ya USA Inayosemwa Itakuwa Vita ya Tatu ya Dunia

$
0
0
Miezi kadhaa iliyopita tumesikia majigambo ya hapa na pale juu ya URUSI kuhusishwa na maandalizi ya VITA KUU YA TATU YA DUNIA, na inaposemwa vita ya dunia zinakuwa pande mbili zinazopingana kufuatana na mienendo mbali mbali, na pande zinazopingana ni lazima ziwe na nguvu ya juu sana duniani na zinakuwa na wafuasi ambao ni vi nchi omba omba vya ulimwengu wa tatu, na wafuasi wengine ambao wanakuwa na visa dhidi ya taifa fulani,

Kwa wanaoangalia mzozo juu juu watadhani vita ya Tatu endapo ikitokea watahusika U.S.A na RUSSIA tu, hapana bali nchi zote ombaomba ikiwemo ya kwako iliyosema haitafungamana na upande lazima iumie,

SABABU ZA KWANINI URUSI HAWEZI ANZISHA VITA DHIDI YA MAREKANI NA KUPELEKEA VITA YA TATU YA DUNIA NI KUWA ANAJUA ATSHINDWA VITA HIYO NA SABABU ANAZOJUA ZITAMFANYA ASHINDWE NI ZIFUATAZO,

1, USA ni mratibu namba moja ulimwenguni kwa kuratibu vituo na kambi za kijeshi kila sehem duniani(millitary bases) kwa idadi 38, ambazo zina mafunzo sahihi, ya vitendo , vimeimarishwa kwa rasilimali watu(wanajeshi), wana usalama na ulinzi, mfano pale ujerumani RAMSTEIN AB na idadi wa wataalamu wa mbinu za kijeshi 9,200. na kwenye nchi nyinginezo pia, hii inampa nguvu USA kuwa na uhakika wa kushinda vita endapo haitakuwepo kuhusika kwa matumiz ya mabomu ya nyukilia,

fungua
List of United States Army installations in Germany - Wikipedia

na mifano zaidi ya bases za nje ni kamaifuatavyo
ushirikiano wa USA na nje (over seas)
Pine Gap Joint Defence Space Research Facility, Alice Springs, Northern Territory, Australia—used by United States armed forces, and CIA, in partnership with the Australian Defence Force and the Australian intelligence services.
War Reserve Stocks are located in many nations.
2. IDADI YA WANAJESHI
idadi ya wanajeshi wa USA waliotiyari kwa lolote ni 145,215,000
ukilinganisha na idadi ya wanajeshi wa RUSSIA ambao ni 130,000,000

3.TEKNOLOJIA
----AIRCRAFT CARRIER STRENGTH,
USA Wana air craft 19 zenye uwezo wa kwenda popote baharin na zikapiga kambi kikawa kama kisiwa na shughuli za kijeshi zikawa based hapo bila kuomba hifadhi, lakin URUSI ana 1 nayo ndogo
---Attack aircraft represents the fixed-wing bomber and ground attack force of a given country
hizi aircraft nimuhim sana katika jeshi lolote lile ambalo liko tiyari kupigana kimataifa na kupata ushindi, hawa wote wawili wanayo haya ma aircraft na takwimu hizi
USA...........2,785
RUSSIA......1,438
Kwa kifupini kwamba marekani anazo mara mbili ya RUSSIA

-----Fighter Aircraft
Wakati FIGHER AIRCREFT za URRUSI ni 751 ambazo ni za zamani miaka ya 90, USA ana 2,308 ambazo ni za kisasa na invisible ambazo score of stealthiness, armament, speed, range, maneuverability and technology ni kubwa na za kisasa.
mfano -Nr.1 Lockheed Martin / Boeing F-22 Raptor
-Nr.2 Lockheed Martin F-35
-Nr.3 Boeing F/A-18E/F Super Hornet

USA 2,308
RUSS 751
SUB MARINES
USA ---75
RUS---60

MLRS (Multiple Launch Rocket System) Strength, HAPA RUSSIA ANAZO NYINGI KUMZIDI MAREKANI,
RUSSIA-----3,793
USA------- 2,309

4. Uwekezaji na bajeti katika jeshi, hapa ndipo majeshi yanaimarishwa kuimarisha vifaa na teknolojia, na kuongeza ari ya kujituma kwa wanajeshi husika katika mazingira yeyote yale yanayoendana na jeshi kwa ujumla, inaoekana jeshi la marekani linapata maboresho na uwekezaji zaidi mara 12 ya lile la URUSI,
USA 581,000,000,000 USD
RUSSIA 46,600,000,000 USD
HII inaonesha dhahiri kuwa america kujiandaa kijeshi ni suala la muendelezo siyo kama nchi zinazoibuka kwa muda tu na kutisha kidogo zikapotea, Upande wa urusi yeye masuala ya kuwekeza kwenye jeshi si sana kama marekani, anategemea teknolojia ya ICBM ambayo ni moja yenye nguvu waliyo nayo na wanaiangalia kwa umakini maana ikifeli hiyo hawana nyingine na hii ni kutokana na kwamba hawajawekeza sana kuibua njia mbadala za kiteknolojia katika jeshi.

5.USHIRIKA KIJESHI NA MAGWIJI/ ALLIANCES

WASHIRIKA WA USA NA NGUVU ZAO KIJESHI
---Nje ya ushirikiano na NATO, pia kuna nushirika kijeshi zaidi na nchi zifuatazo
A. ISRAEL, kila mmoja duniani anatambua nguvu ya Israel kama masuala ya kijeshi na intelligensia , hasa wako na moyo wa kukamilisha jambo wanalopania hawajali gharama zitakazo tumika, kujitoa kwa namna hii kunaamsha ari ya kuleta ushindi,
Nguvy ya ISRAEL kijeshi ni nafasi ya 16 ikiwa GPF ranking points 0.3591
B. GERMANY, hii nchi ni mshirika wa kijeshi wa marekani , Iko nafasi ya 9 GPF 0. 2646
C. ITALY
D. FRANCE
E. ENGLAND
F . TURKEY
G.SOUTH KOREA
H. CANADA
I. NETHERLAND
J. NORWAY



WASHIRIKA WA URUSI NI WALE AMBAO WANA NGUVU LAKIN SI SAWA NA WASHIRIKA WA USA
USHIRIKA UNAOWEZA KUMSAPOTI URUSSI
A.NORTH KOREA ,
B. LEBANON
C. IRAN
D. SYRIA
na vinchi vingine vidogo vidogo vya kiarabu vyenye chuki na marekani,

WASHIRIKA WENYE NGUVU AMBAO WATAJOIN UPANDE MMOJA WAPO KUTOKANA NA INTEREST AU WASIJOIN KABISA
1. CHINA anaweza asijihusishe kabisa na Vita ili kuepuka kuteteresha uchumi wake maana wao wanaangalia fursa tu, lakin pia wanaweza wakaamua nkutoi sapoti MAREKAN kutokana na kwamba JAPAN Atamsapoti , na wana chuki za mda mrefu na JAPAN, na Pia hawatamjoin URUSI kuhofia kupoteza SOKO lao nchini USA,
2. INDIA haeleweki japo ana nguvu kubwa kijeshi na ataana kusoma upepo, wa VITA inendaje,
3. BRAZIL vile vile hana upande maalum,


ukipitia hapa ukapata uelewa wa kutosha unaweza ukagundua kuwa HAKUTAKUWEPO NA VITA YA TATU YA DUNIA MAANA ANAYEONEKANA KUTAKA IWEPO AKIFIKIRIA HAYO HAPO JUU ANASITA,
NA AKIAMUA ATOKE KWA NJIA YA NYUKILIA , AKUMBUKE USA NDO WENYE NYUKILIA SANA , NA WAMEKUWA WAKI HADAA DUNIA KUWA HAWANA NYUKILIA KUMBE WANAZO NA PUTIN ANALIJUA ILO, PIA UKIZINGATIA NA SABABU ZILIZOPELEKEA KUVUNJA MKATABA WAO NA USA JUU YA SUALA LA KUHARIBU NYUKILIA

By Kevin Isaya

Maneno ya Diamond kwa Harmonize Baada ya Kushindi Tuzo ya AFRIMMA

$
0
0
Tuzo za AFRIMMA ambazo hutolewa kila mwaka kwa Waafrika mbalimbali waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali hasa za burudani, zimetolewa Dallas Texas Marekani leo ambapo kwenye list yote Watanzania walioshinda ni watatu.

Watanzania walioshinda ni Dj D Ommy wa CloudsFM kupitia show mbalimbali ikiwemoXXL na AMPLIFAYA ambapo ameshinda tuzo ya Dj bora Afrika, mwimbaji Harmonize akishinda tuzo ya msanii bora chipukizi Afrika 2016 huku Diamond Platnumzakishinda ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.

Sasa miongoni waliotoa pongezi kwa Harmonize ni Diamond Platnumza ambae kupitia instagram alipost picha na kuyaandika haya:
Hii picha inanikumbusha mwaka jana ulipokuja nipokea airport kutokea@afrimma …ukaniuliza “hivi ipo siku nami nitachaguliwa tunzo yoyote ya kimataifa”….nikakwambia “Ukifanya kazi kwa bidii’
‘Ukimuheshimu kila mtu, ukamuamini na kumuomba Mwenyez Mungu basi Mollah atakufungulia ndoto zako….na leo hii kweli Tunafurahia Ushaindi wako wa Msanii Bora Chipkizi Africa….. Hongera sana @harmonize_tzna shukran sana sana kwa Mashabiki zetu pendwa kwa kura na @Afrimmakwa kuendelea kuvinyanyua vipajia vya Africa🙏’-Diamond Platnumz
Viewing all 2111 articles
Browse latest View live