Quantcast
Channel: Siasa Huru
Viewing all 2111 articles
Browse latest View live

Wanaotumia Kope Bandia Hatarini Kupata Upofu wa Macho

$
0
0
Wanawake wanaotumia kope bandia wanahofiwa kuwa na hali ya hatari ya kupata upofu wa macho kutokana na gundi wanazotumiwa kutumia kope hizo kuripotiwa kuripotiwa kuwa na athari kwenye macho yao.

Tahadhari hiyo imetolewa na mratibu wa huduma ya macho ya mkoa wa Iringa, Dk George Kabona,alipokuwa akitoa tathmini ya huduma ya macho ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya afya ya macho duniani.

“Ningependelea wasipende kuzivaa kama fasheni ya kawaida,kwasababu zina madhara sana. Kwasababu hizo kope unabandika kwa kile kitu ambacho ile chemical ya kubandikia ndio huwa inaogopwa zaidi kuliko hata kope zenyewe. Ingekuwa labda unazibana na stapler hivi labda lakini kuna kitu unabandikia ile kitu ndio jicho halikitaki kama kinaendelea kukaa pale muda mrefu,”alisema Kabona.

“Pia hupelekea uoni hafifu. Pia linaweza likawapelekea watu shida ya kuona kwasababu uoni hafifu kuna ule mkali na uoni hafifu wa nafuu. Ukiwa ule mkali utakuletea shida kwenye shughuli zako za kila siku. Ukiwa katikati kama unaangalia TV, ukiwa unataka kumuona mtu unasogea maisha yanaweza yakaendelea. Lakini kuna ule mkali kabisa unakaribia na upofu unahitaji huduma.”

Mohammed Dewji Amwaga Sifa Hizi Kwa Diamond Platnumz

$
0
0

Miongoni mwa bilionea wa Afrika aliyekuwa Mbunge wa Singida na CEO wa MeTLGroup, Mohammed Dewji, afunguka kuhusu Diamond platnumz.

 Dewji amemwaga sifa kwa mwanamuziki Diamond Platnumz kuwa ni miongoni mwa wanamuziki wa wakubwa barani Afrika lakini mwenye uwelewa mzuri.
Kupitia account yake ya Instagram, Mohammed Dewji, aliweka picha yake akiwa na Diamond na kuandika maneno hayo kwa Kingereza yaliyo someka hivi..

Today afternoon with @DiamondPlatnumz

 One of Africa’s biggest and smartest artists in the music industry #TanzaniansUnite

Rais wa Nigeria Amjibu Mkewe...Adai Mkewe ni was Kwake Jikoni na Chumbani na si Vinginevyo

$
0
0

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amejibu onyo kutoka kwa mkewe ambaye alikuwa ametahadharisha kwamba hatamuunga mkono uchaguzi mkuu ujao iwapo hatafanya mabadiliko serikali.

Bi Aisha, kwenye mahojiano na BBC, alikuwa amedokeza kwamba mumewe amepoteza udhibiti wa serikali.

Bw Buhari kwa sasa yumo kwenye ziara rasmi nchini Ujerumani na kwa mujibu wa shirika la habari la AP, amemjibu mkewe wakati wa kikao cha wanahabari akiwa pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

"Sijui mke wangu ni wa chama gani, lakini najua yeye ni wa kwangu jikoni na sebuleni na chumba hicho kingine," amesema Bw Buhari.

Kwa mujibu wa AP, kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwaka jana amesema pia kwamba na ujuzi na uzoefu zaidi ya mkewe katika siasa.

"Kwa hivyo, nina ujuzi kushinda yeye na watu wengine wa upinzani, kwa sababu mwishowe nilifanikiwa. Si rahisi kuridhisha vyama vyote vya upinzani nchini Nigeria au kushiriki serikalini."

Wandishi wa Mwananchi Wapata Ajali

$
0
0

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Mkoani Mwanza, Peter Saramba na Mpigapicha Michael Jamson wamepata ajali eneo la Kimbu B, Wilaya ya Bariadi wakiwa wanatoka Simiyu kwenye sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere zilizoambatana na kuzima mwenge.

Akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya ajali hiyo, Saramba alisema  watu wawili wamefariki papohapo katika ajali hiyo wakati yeye akiwa amelazwa katika hospitali ya Mkula Wilaya ya Busega akipatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyoyapata..

“Ajali ilikuwa mbaya sana,ila namshukuru Mungu nipo mzima ingawa nimepata majeraha madogomadogo, lakini tumeletwa hapa Busega katika hospitali ya Kikula kwa ajili ya kupatiwa matibabu, na tayari madaktari wanatuhudumia hapa” alisema Saramba.

Mwanaume Ashikiliwa na Polisi Kwa Kumbaka Mtoto wa Miaka 6

$
0
0

KENYA: Kijana mmoja(20) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumjeruhi sehemu za siri mtoto wa kike wa miaka 6.

Mtoto huyo amefanyiwa unyama huu akiwa njiani akitoka shule ambako anasoma darasa la awali.

Baada ya kusimulia mkasa mzima wanakijiji walianza kumsaka kijana huyo na hatimae wakampeleka katika kituo cha Polisi kwa taratibu za kisheria.

Aidha mtoto huyo amelazwa hospitali akisubiri kufanyiwa upasuaji.

Damu Kusafirishwa na Ndege Zisizo na Rubani Rwanda

$
0
0

Damu kusafirishwa na ndege zisizo na rubani Rwanda*
Maeneo mengi ya Rwanda yana milima na misitu hivyo huwa vigumu kusafiri kwa kutumia barabara
Huduma ya kusafirisha damu na vifaa vingine vya kimatibabu kwa kutumia ndege zisizo na rubani, inazinduliwa leo nchini Rwanda.

Huduma hiyo ni ya kwanza ya aina yake duniani.

Ndege zisizo na marubani zitakuwa zikipaa moja kwa moja hadi eneo ambalo damu inahiajika nchini Rwanda, na kisha kurejea kituoni.

Badala ya kutua ndipo ziwasilishe kifurushi chenye damu, kifurushi hicho kitarushwa ardhini salama kwa kutumia mwavuli au parachuti.

Teknolojia hiyo inaleta matumaini ya kuwasilisha damu haraka na kwa njia salama ukilinganisha na awali ambayo njia ya kutegemewa pekee ilikuwa barabara, nyingi ambazo ambazo hali yake ni mbaya.  Vifurushi vitakuwa vikirushwa ardhini kwa kutumia mwavuli au parachuti. Ndege hazitahitaji kutua.
Kampuni ya Marekani ya Zipline ndiyo itakayoendesha mradi huo.

Wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ni wahandisi ambao awali walifanya kazi katika kampuni maarufu za kiteknolojia kama vile Space X, Google, na Lockheed Martin.. Mwanzoni, ndege hizo zitatumiwa kusafirisha damu, maji ya damu na dutu inayogandisha kioevu.

Ndege hizo zinaweza kuruka na kupaa zikiwa futi 500 (mita 152) juu ya ardhi kuzuia kugongana na ndege kubwa za kawaida zinazobeba abiria na mizigo.

Ndege hizo zitakuwa zinahudumu eneo la umbali wa hadi kilomita 150 (maili 93), ingawa zina uwezo wa kwenda umbali maradufu ya umbali huo.  Ndege hizo za Zipline zikirushwa angani kutoka kwenye kambi iliyopo karibu na mji wa Kigali
Ndege hizo zinatumia nguvu za umeme kutoka kwenye betri na hutumia teknolojia ya GPS kuziongoza kufika maeneo yanayotakikana.

Zitakuwa zikituma maeleo kwa wahudumu kwenye kambi ya ndege hizo na pia wahudumu wasimamizi wa safari za ndege Rwanda kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu.
Kwa kuanza, ndege 15 zitakuwa zikifanya kazi.
Ndege hizo, ambazo kwa kifupi zinafahamika kama 'Zip', zina uwezo wa kupitia hata kwenye upepo wa kasi ya kilomita 30 kwa saa (19mph) au mvua ndogo hali ikibidi.  Wakati wa kufanyiwa majaribio kwa teknolojia hiyo......

Wanawake Achaneni na Waume wa Namna Hii, Wakimbieni Kama Ebola ni Hatari Sana

$
0
0
Kumezuka wimbi kubwa la wanaume wenye ndoa kuwaingilia wafanyakazi wao kimwili. hili ni jambo la aibu na la kusikitisha sana. wanaume wanaotenda jambo hili ni wanaume wa hovyo kabisa duniani. hawa mi huwa nawafananisha na fisi ambaye yeye anafukuzia mizoga na wanyama dhaifu. mwanaume wa kweli huwezi mdandia housegal wako hata iweje. unaonesha udhaifu kuwa sasa umeishiwa skills na unaamua kudandia mizoga.ashakum si matusi. mizoga kwa maana ya kuwa house gals wengi wanakuwa hawana uwezo wa kuwakataa. hasa kwa ahadi zenu za kijinga kuwaongezea salary au kuwahonga 10,000-20,000 na sometime 5,000

jamaa mmoja tupo naye mtaani amechana na mkewe kwa kisa cha kutembea na kumtia mimba msichana wake wa kazi. yule mama amesema wazi hawezi mrudia mumewe hata kwa bunduki.anasema ni uchavu na kuishiwa sera kwa mumewe.pamoja na jamaa kuwa ni tajiri sana mke ameamua kuacha mali zote na kwenda kupanga chumba kimoja kuanza maisha mapya. amebembelezwa sana. sana na watu wa aina yote na jamaa amesema hata yupo tayari kumnunulia gari alitakalo kumfanya amsamehe.mke kamwambia atakuwa na mdanganya maana hatoweza tena kufanya naye mapenzi so ndo yao automatically itakuwa imekufa.

nikajiuliza inakuaje mwanaume mzima unamrubuni dada wa kazi unamalalia? unampumulia? unamwegamia? nao ni binadamu sikatai basi ukiona hali ipo hivyo si mwondoe kazini then mkafanyie uhuni wenu huko? nyumba moja unakuka dada wa kazi?kweli??????

dada zangu nawaambia usikubali kuishi na mwanaume aliyeishiwa sera kiasi hicho. ambaye anategemea mteremko..huyu ni hatari maana sasa amekuwa kama fisi. hachagui habagui atakayezikwa anye hamjui.

kuna wanaume kweli wao hawana viwango vya mwanamke wa kutembea naye. awe mweupe,mweusi,mnene,mwembamba,mrefu,mfupi yaani yeyote yule ili mradi tu awe na nani.....wanaume wa namna hii ni wenye ulemavu wa mbaya sana na hawa mara nyingi wanakuwa ni mafisi. lazima mwanaume uwe na kigezo. mwanaume wa namna hii anaweza kutembea na hata ndugu zako au zake.

jaman njaa hii njaa gani? hadi mnakula mizoga? na nawapenda kuwapa tahadhari hii. HAKUNA BINADAMU RAHISI KUPATA MIMBA KAMA HOUSE GIRLS. MIMBA ZAO ZIPO KARIBU SANA. SIJUI WAMEUMBWAJE? na utafiti unaonesha ni nadra sana kupata HOUSE GIRL MGUMBA. msije sema sikusema

Kampeni Chafu Zatikisa CCM, Moto wawaka Kashfa ya Makontena Mia Bandarini...Magazeti ya leo

$
0
0


Kampeni Chafu Zatikisa CCM, Moto wawaka Kashfa ya Makontena Mia Bandarini...Magazeti ya leo

Mrembo Naj Aelezea Jinsi Alivyokutana na Mama yake Baraka Da Prince na Kukaa Naye Siku Nne

$
0
0
Mrembo kutoka Bongoflevani Naj ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mkali anayemiliki mdundo wa ‘Nisamehe’ Baraka the Prince, Leo October 15 anazichukua headlines baada ya kuelezea exclusive baada ya kwenda nyumbani kwa mpenzi wake na maneno waliyoongea na mama mkwe wake.

‘Unajua Idea ya kwenda kwa kina Baraka aliitoa Baraka mwenyewe, nilivyosikia ananiambia vile nilijisikia raha sana, nimekaa kama siku nne  Mwanza na sikutegemea jinsi walivyonipokea maana nilijua wataniona mimi ni culture za kizungu sana‘>>>Naj
‘Tumeongea mambo mengi sana na mama yake baraka vingine ni siri yangu lakini vingine ni kuhusu vyakula anavyopenda baraka na ambavyo avipendelei, pia aliniambia kuwa baraka huwa hapendi kula nyama‘ Naj

Majina Ya Wanafunzi Waliopata Mkopo Mwaka Wa Masomo 2016/2017----(Awamu ya Kwanza)

$
0
0
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu wametangaza majina ya wanafunzi waliopata mkopo 2016/2017 awamu ya kwanza.

Hapa ni link ya kuangalia kama umepata au laah unaandika namba ya form 4 na code walizokupa hapo.

Kumbuka format ya form 4 no. ni s0001.0001.0001 na sio s0001/0001/0001

Link hii hapahttp://olas.heslb.go.tz/index.php/allocation/allocations/fresher_login
  
Chini limeambatanishwa FILE la Orodha ya Waliopata Mkopo 2016/17  

1.First List Of Loan Beneficiaries For Academic Year 2016/2017. <<Click here>>
  


2.First Year Loan Allocations Breakdown for 2016/17 . <>

Picha za Samaki Aina ya Nyangumi Aliyekufa Ufukweni Bahari ya Hindi Kilwa

$
0
0
Samaki mkubwa amekutwa amekufa jana katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Bandari ya Kilwa, Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa samaki huyo alianza kuonekana kuanzia jana akielea baharini lakini hawakujua kama alikuwa amekufa hadi leo aliposukumwa hadi kwenye ufukwe wa bahari.

Wakazi hao wanaeleza kuwa samaki huyo ana urefu wa futi 30.


Tazama Video DC Richard Kasesela Akionyesha Jinsi ya Kushika Bunduki na Kupambana na Adui Katika Vita

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akionyesha jinsi ya kushika bunduki na kupambana na adui uwapo katika uwanja wa mapambano.

Ushikaji wa bunduki wakati wa pambano huwa ni changamoto kwa sababu usipokuwa umejiweka sawa ukifyatua risasi kutokana na msukumo unaweza kuanguka.

Katika video hii, baada ya DC Kasesela kumaliza anapongezwa na Wanajeshi waliokuwa katika mazoezi hayo kwa namna alivyofanya vizuri. Itazame video hapa chini.

Tamko la TFF Kuhusu Taarifa ya Kukodishwa Kwa Yanga

$
0
0
Shirikisho Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeiandikia barua uongozi wa Young Africans Sports Club kutaka ufafanuzi wa kile kinachoripotiwa kuhusu Bodi ya Wadhamini kuingia mkataba wa kuikodisha kwa Kampuni ijulikanayo kwa jina la Yanga Yetu Limited.

Kimsingi TFF haipingi mabadiliko ya aina yoyote, badala yake inataka kujua kama taratibu hasa zinazohusiana kisheria kama zimefuatwa hivyo sasa imeitisha mkataba huo kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans, Bakara Deusdedit ili kuona kile kinachoelezwa kuhusu mfumo wa uendeshwaji na umiliki wa klabu hiyo yenye zaidi ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.

“Msimamo wa TFF  ni kwamba klabu ya Yanga ipo kama ilivyokuwa kwa mujibu wa taratibu za TFF, CAF na FIFA hadi hapo tutakapopopata barua kutoka Young Africans na wanatambua uongozi wa Mwenyekiti Yussuf Manji na Kaimu Katibu Mkuu Deusdedit Baraka,” amesema Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine.

TFF imekuwa ikipokea barua kutoka kwa wadau mbalimbali wa Yanga wakihoji taratibu au hatua zinazoendelea katika mfumo wa umiliki na uendeshwaji wa timu hiyo. Mbali ya hatua hiyo, Alhamisi iliyopita ya Oktoba 6, 2016 vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa na taarifa kuhusu muhtasari wa mkataba wa Yanga wa kukodishwa na kampuni ijulikanayo kama Yanga Yetu Limited.

Mbali ya misukumo hiyo, pia TFF haikuridhika na majibu ya Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans, Bakara Deusdedit ambaye alipoandikiwa barua kwa mara ya kwanza Agosti 30, 2016 alitoa majibu kwamba awasiliane na wajumbe wa Bodi ya Udhamini.

Mwesigwa amesema wanataka kuona kilichopo kwenye mkataba kabla ya kushauri uongozi ili kuangalia kama vinakwenda sambamba na matakwa ya TFF, CAF na FIFA ili kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakiendelea kwani wengine wamefika hatua ya kuomba idhini ya TFF hata kwenda kuwaona viongozi wa serikali.

Mwesigwa alisema wanataka kujua pia nani anamiliki na nani anaendesha timu na umiliki wake ukoje kwa maana hizi timu za Simba na Yanga zinagusa nyoyo za watu wengi na taratubu za uhamishaji umiliki wake ukawa wa wazi-hadharani.#

“Mambo ya kubadilisha uendeshwaji unatakiwa kufuata taratibu ikiwa ni pamoja kuenenda sawa na katiba ya klabu, kamati ya utendaji ifahamu, mkutano mkuu uridhie ili kujua nini kinauzwa na nini kinakodishwa ikiwa ni kwenye level (hatua) ya klabu.

“Kama itakuwa nje ya utaratibu wetu wa uendeshaji wa klabu kamati ya sheria na kamati ya utendaji watafanya kazi na kama watakuwa wamefuata taratibu inaweza isifike huko kwenye CAF na FIFA,” alisisitiza Mwesigwa.

Mwesigwa alisema TFF itaendelea kuwasiliana na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit au Mwenyekiti, Yussuf Manji kwa mambo yote yanayohusu sera na mipango na siyo Bodi ya Wadhamini kama ambavyo Baraka alielekeza.

KUHUSU SIMBA SC

Mwesigwa alisema, katika mawasiliano ya barua ya Agosti 30, 2016 Simba walitoa majibu ya kuwa tayari wako  kufanya hivyo wakati wowote wakihitajika na kuna wakati walikosa muda kwa sababu ya shughuli zao mbalimbali za klabu.

Moto Wawaka Kashfa Kontena 100 Bandari

$
0
0
SIKU moja baada ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, kusema kontena 100 zimeondolewa Bandari ya Dar es Salaam bila kukaguliwa na Shirika la Viwango (TBS), moto kuhusiana na suala hilo umezidi kuwaka.

Hali hiyo imejidhihirisha kutokana na taarifa kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) haikuhusishwa vya kutosha katika utoaji wa taarifa sahihi juu ya suala hilo huku TBS wakidai kuwa hadi kufikia jana, tayari wafanyabiashara 10 walishajitokeza kwao kwa nia ya kutoa maelezo.

Akiwasiliana na Nipashe jana, Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, alielezea kushangazwa na taarifa zilizoelezwa kuhusiana na kontena hizo.

Aidha, Kakoko alisema hali hiyo ya kutolewa maelezo bila kutaka taarifa kwao ni sawa na ‘kukwepa kupata taarifa sahihi kutoka sehemu sahihi’.

Maadhimisho ya Nyerere Yafanyika Bila Familia ya Nyerere

$
0
0
Maadhimisho ya miaka 17 ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika jana mjini Bariadi mkoani Simiyu jana bila kuwapo wa familia ya mwasisi huyo wa Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema Oktoba 5, mwaka huu Mama Maria Nyerere alikuwa miongoni mwa waalikwa katika sherehe hizo na mipango kwa ajili ya malazi yake na msafara ilikuwa imeandaliwa.

Katika mipango ya awali, mama Maria na msafara wake alipangiwa kufikia katika nyumba za halmashauri ya mji wa Bariadi zilizoko eneo la Nyamuata kabla ya kuhamishiwa katika hoteli mpya ya Sumayi katikati ya mji wa Bariadi.

Meneja wa hoteli hiyo, Mabula Mapolu alithibitisha ugeni wa Mama Maria kupangiwa kufikia hotelini lakini, baadaye walipewa taarifa kuwa ugeni huo usingefika na badala yake

hoteli hiyo ikapangiwa wakuu wa mikoa na wilaya kutoka Zanzibar, ambao nao walilazimika kuondoka juzi kutii agizo la Rais John Magufuli la kuwataka kurejea kwenye vituo vyao vya kazi.

Akizungumzia sababu za familia hiyo kutofika, mmoja wa watoto wa Mwalimu Nyerere, Madaraka

Nyerere alisema yeye binafsi hakuona mwaliko wa familia kuhudhuria sherehe hizo, akisema huenda ulipokewa na mwana familia mwingine kwa kuwa familia yao ni kubwa.

“Yawezekana mwaliko ulipokewa na mmoja wa wanafamilia kutokana na familia yetu kuwa kubwa. Lakini aliyeupokea akapata hudhuru na

kushindwa kuhudhuria; Hii haimaanishi kuwa Serikali haikutoa mwaliko,” alisema Madaraka akiwa Butiama.

Familia hiyo jana ilishiriki ibada maalumu katika Kanisa Katoliki Butiama ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi kadhaa wa Serikali, wakiwamo Mkuu wa mkoa huo, Dk Charles Mlingwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyetajwa kumwakilisha Rais John Magufuli pamoja na wakuu wa wilaya za mkoa wa Mara.

Mbunge wa Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya pia ni miongoni mwa waliohudhuria ibada hiyo.

Mbali na maadhimisho ya kitaifa yaliyoambatana na sherehe za kuzima mwenge, ilifanyika ibada katika

Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yohana mjini Bariadi iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo la Shinyanga, Liberatus Sangu.


Askofu Sangu aliwataka viongozi wa Serikali

kuyaenzi kwa vitendo aliyoyaacha Nyerere kwa kupiga vita na kukemea rushwa, ubadhirifu, ubaguzi wa kiitikadi, kidini, kikabila na maeneo huku kila mmoja akidumisha amani, utulivu.

Aliwaomba Watanzania kila mtu kwa imani yake kushirika kumwombea Mwalimu Nyerere kutangazwa kuwa mwenye heri katika mchakato unaoendelea ndani ya Kanisa Katoliki.



Dk Shein

Akihutubia taifa katika kumbukumbu hiyo, Rais wa Zanzibar, Dk Ally Mohamed Shein aliahidi kuwa Serikali itayaenzi yote yaliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere akitaja ulinzi na usalama, amani, upendo, mshikamano na umoja wa kitaifa kuwa ni miongoni mwa hayo.

Kiongozi huyo alisisitiza msimamo wa Serikali wa kutokubali msaada yenye masharti ya kutweza, kudhalilisha utu na uhuru wa Watanzania, badala yake aliahidi kuwa Tanzania itashirikiana na mataifa yote na kupokea misaada isiyo na masharti magumu.

Akizungumzia uwezeshaji kwa vijana, Dk Shein alisema Serikali itaendelea kutekeleza sera ya kuweka mazingira bora na kuwawezesha vijana kuanzisha miradi ya kiuchumi kulingana na fursa zinazopatikana katika maeneo yao huku akikemea tabia ya baadhi ya vijana kushinda vijiweni bila kufanya kazi.

Katika hotuba yake Dk Shein alisisitiza msimamo wa Serikali za Muungano na Zanzibar katika kupambana na ubadhilifu na rushwa ili kuboreshwa na kuimarisha huduma za kijamii katika nyaja zote.

Kiongozi wa mbio za Mwenge, George Mbijima alitaja tishio la kiusalama kutokana na wahamiaji

BOT Yatetea Matumizi ya Dola...Wadai Sio Chanzo cha Shilingi Kushuka

$
0
0
BENKI Kuu Tanzania (BoT), imesema matumizi ya fedha za kigeni kama vile dola, pauni na Euro, hayasababishi kushuka au kuifanya shilingi ya Kitanzania kutetereka.

Badala yake BoT imesema sababu za kushuka au kuyumba kwa sarafu ya nchi, mbali na mfumuko wa bei ni nakisi ya mapato na matumizi ya nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi, Johnson Nyella, alisema hayo baada ya Nipashe kutaka kujua benki hiyo imetekelezaje agizo la aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, alilolitoa bungeni mwaka 2007 kutaka miamala yote ya kibiashara isifanyike kwa fedha za kigeni, ikiwamo dola.

Nyella alisema kushuka kwa shilingi hakusababishwi na matumizi ya dola kama imani iliyojengeka miongoni mwa Watanzania.

Mke wa Mrehemu Filikunjombe Aibua Mapya....

$
0
0
Ukiwa umepita mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, mjane, wazazi na wakazi wa jimbo hilo wamefanya ibada ya kumkumbuka ambayo imeibua upya simanzi.

Filikunjombe alifariki dunia  Oktoba 15, 2015 katika ajali ya helikopta iliyoanguka na kulipuka katika Hifadhi ya Taifa ya Selous mkoani Morogoro wakati akitokea Dar es Salaam kwenda Ludewa  mkoani Njombe. Wengine waliokufa katika ajali hiyo ni Egid Nkwera (43), Casablanca Haule (53) na William Silaa, aliyekuwa rubani wa helikopta hiyo.

Akizungumza  wakati wa ibada hiyo, mjane huyo, Sarah alisema: “Huwa namuota mara kwa mara na hali hiyo inanifanya nizidi kumuombea kwa Mungu ampumzishe kwa amani.”

Aliishukuru familia ya marehemu kwa kuendelea kumpa mahitaji muhimu na kusomesha watoto.

Sarah ambaye wakati wa uhai wa mumewe alikuwa mama wa nyumbani, kwa sasa ameanzisha kilimo cha matunda na mbogamboga ili kuongeza kipato chake.

Philip Filikunjombe ambaye ni mdogo wa marehemu, amesema kifo cha kaka yake kimemuachia mzigo wa kutunza familia tatu ikiwamo yake na wazazi  wake (Deo).

Mbali ya kutunza familia hizo, pia anaendelea kusomesha zaidi ya watu 700 ambao walikuwa wakilipiwa ada na kaka yake wakati wa uhai wake.

Mkazi wa Ludewa, Ludende Mgimba alisema kifo cha Filikunjombe kilizima nuru ya maendeleo ya haraka aliyokuwa nayo kwa wakazi wa jimbo hilo.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Ludewa, Juma Madaha amesema anamkumbuka Filikunjombe kutokana na ujasiri na mapenzi aliyokuwa nao kwa wananchi wake.

Ibada hiyo ilifanyika Kanisa Katoliki la Ludewa kuanzia asubuhi na kufuatiwa na chakula cha mchana nyumbani kwa Filikunjombe, Mtaa wa Ibani.

Ukiwa na Simu ya Sumsung 7 Marekani Hawezi Panda Ndege Nayo...

$
0
0
Idara ya uchukuzi nchini Marekani imepiga marufuku simu za Samsung aina ya Galaxy Note 7 kwenye ndege zote nchini humo.

Hii ni baada ya visa vya simu hizo kushika moto kuripotiwa.

Abiria hawataruhusiwa kubeba simu hizo ndani ya ndege au hata kwenye mizigo yao wakiingia au kutoka Marekani kuanzia Jumamosi saa 16:00 GMT.

Idara ya uchukuzi ya Marekani ilikuwa awali imewashauri abriia dhidi ya kuweka simu hizo kwenye mikoba yao.

Samsung ilitangaza kwamba haitaunda tena simu hizo wiki hii.

"Tunatambua kwamba kupigwa marufuku kwa simu hizi ndegeni kutatiza baadhi ya abiria, lakini tunazingatia sana usalama wa watu walio ndani ya ndege," karibu wa uchukuzi Anthony Foxx alisema kupitia taarifa.

Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.

Walipewa simu mpya ambazo zilidaiwa kuwa salama

Lakini taarifa zilitokea baadaye kwamba hata simu hizo zilizodaiwa kuwa salama zinashika moto.

Familia ya Nyerere Gizani

$
0
0
MAMA Maria Nyerere na familia yake hawakuhudhuria Sherehe ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ilizofanyika Bariadi mkoani Simiyu jana.

Kumbukumbu hiyo hufanyika kila mwaka tangu Mwalimu Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania alipofariki tarehe 14 Oktoba 1999 alipokuwa kwenye matibabu nchini Uingereza.

Licha ya Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuarifu kwamba, Mama Maria Nyerere, mke wa mwalimu angehudhuria sherehe hizo, hakwenda.

Taarifa ya Mtaka aliyoitoa tarehe 5 Oktoba mwaka huu ilieleza kuwa, Mama Maria Nyerere pamoja na familia yake, wangefikia Nyamuata ambazo ni nyumba za Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Baadaye Mtaka alibadilisha makazi ya Mama Maria angefikia kwenye Hoteli ya Sumayi jambo ambalo lilithibitishwa na viongozi wasimamizi wa hoteli hiyo.

Pamoja na taarifa za Mtaka pia uthibitisho wa uongozi wa Sumayi kwamba, Mama Maria Nyerere angefikia kwenye hoteli hiyo kwa ajili ya kumbukumbu hiyo, hawakufika.

Familia ya Mwalim Nyerere imekuwa ikishiriki maadhimisho hayo ambayo ni ya kitaifa kwenye maeneo mbalimbali tangu kufariki kwa Mwalimu Nyerere.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Mwalimu Nyerere zinaeleza kutopata mwaliko wowote kutoka katika Serikali ya Rais John Magufuli ili kuhudhuria sherehe hizo.

Wakati serikali ikiendelea na maadhimisho yake mkoani Simiyu, familia ya Mwalumu Nyerere ilifanya ibada Maalumu katika Kanisa la Katoliki, Butiama.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Sospiter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini na kwamba alimwakilisha Rais John Magufuli.

Wengine waliohudhuria ni Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini na Shyrose Bhanji Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (AELA).

Chanzo: Mwanahalisi

Mbatia: Uhakiki wa Vyeti Feki Uanzie Kwa Rais na Viongozi Wengine

$
0
0
Mhe. James Mbatia (MB) Vunjo, na Mwenyekiti Taifa NCCR. Ametaka zoezi la uhakiki wa vyeti feki ni vyema likanzia kwa Rais na viongozi wengine.

Binafsi naunga Mkono hoja ya Mhe.Mbati kwa sababu mbili tu.

1.Kiongozi hutakiwa kuongoza kwa Mfano, tulitegemea akianza Rais, watafuata na viongozi wengine wote, PM, VP, W. N/W, RC, DC, Wabunge hadi Madiwani.

Aidha, kuna mazoezi mengi hapo awali yalianzishwa na Rais na viongozi wengine Tuliona wakati wa kampani ya UKIMWI na Malaria No More, Tuliona Utambulisho wa makazi, Tuliona kwenye BVR na NIDA.

Ikumbukwe kuwa, JPM alikuwa mastari wa mbele, kwa maana wa kwanza katika Zoezi la UHAKIKI WA SIRAHA Mkoa wa Dar.

2. Kuonyesha uhalali wa zoezi husika, kuwa kama zoezi likianza na Viongozi mara nyingi huchukuliwa ni serious na ni zoezi halali lisilo la kibaguzi kwa baadhi ya kada tu.

Kwani Mpaka sasa kuna baadhi ya Mawaziri inasemekana wanatumia majina fake, so uhalali wa zoezi hili upo wapi?

My Take:
Zoezi lianze kusafisha Nyumbani kwanza ( Baraza la Mawaziri & vigogo)

Source: Gazeti la Mtanzania.
Viewing all 2111 articles
Browse latest View live