Quantcast
Channel: Siasa Huru
Viewing all 2111 articles
Browse latest View live

BURUNDI Imejiondoa Mahakama ya Makosa ya Jinai ICC, Bado Wana Kesi hii….

$
0
0
Wiki hii nchi ya Burundi inazimiliki headlines za kutangaza kuwa bunge la nchi hiyo limepiga kura ya kujiondoa uanachama wake kwenye mahakama ya makosa ya jinai duniani ICC, Ripoti mpya kutoka mahakama hiyo zimesema kuwa Burundi imefanya haraka mno uamuzi huo, wakati tayari ina kesi ya kutumia majeshi yake kama chombo cha ukandamizaji.

Ikumbukwe kuwa baraza la Seneti limepiga kura ya serikali ya Burundi kujiondoa kuwa mwanachama wa ICC na tayari taarifa imemfikia Rais Pierre Nkurunziza kwaajili ya kutia saini.

Hii itakua ni kwa mara ya kwanza kwa mahakama hiyo kukutana na uamuzi wa nchi kujiondoa ingawa ripoti zinasema uamuzi huo hauizuii Burundi kutofunguliwa mashitaka mbele ya mahakama ya kimataifa.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa ICC Bensouda, anasema sheria za Roma zinaeleza kwamba uamuzi wa kujiondoa ICC unachukua mwaka mmoja baada ya tarehe ambayo uamuzi huo utakua umewasilishwa kwa vyombo husika, uamuzi wa kujiondoa hautakua na mabadiliko ya kesi ambazo tayari zinaendelea kushughulikia na taasisi hiyo ya kimataifa hata kama uamuzi huo utabatilishwa.

BAADA ya Wiki 8 Imeripotiwa Drake na Rihanna Wameachana Tena

$
0
0
Hii kwa watu wangu wapenzi wa updates za mastaa wa nchi za nje nikiwazungumzia mastaa kama Beyonce, Rihanna, Jay z na wengine wengi kuhusiana na maisha yao kiujumla hata nja na fani ya muziki, August 28 2016 nilikusogezea hii kutoka kwenye Mtandao wa E News wa Marekani ambao uliripoti mkali wa  Midundo ya hiphop Drake kuwa mapenzini tena na Mrembo Rihanna.

Wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja mara nyingi kwenye mitoko tofauti na kujulikana kuwa wapo tena mapenzini, mabadiliko yalianza kuonekana 0ct 11 2016 ambapo mrembo Rihanna alionekana peke yake akiwa anaelekea club na sio kawaida mrembo huyo kuwa peke yake bila Drake, Enews imeripoti kuwa Drake kwasasa anaonekana kuwa na mrembo mwingine Model ‘India Love’ ambae ametajwa kuwa ni ex wa Rapper ‘The Game’.

Diwani Chadema Anaswa na Dawa za Kulevya, Bunduki

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Diwani wa kata ya Izira, Paschael Silimba (Chadema) baada ya kumkamata akiwa na dawa za kulevya aina ya bangi na bunduki moja aina ya gobole.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Kyando amesema kuwa jeshi hilo lilimkamata Kyando katika eneo la soko kuu ambalo hufanyia biashara yake ya kuuza mifuko ya salfeti, baada ya kupata taarifa na kuamua kumfuatilia.

Alisema kuwa baada ya kumpekua katika vifurushi vya bidhaa hiyo anayoiuza kwa kushirikiana na mkewe, walibaini uwepo wa bangi kiasi cha robo kilo.

“Baada ya kufanya upekuzi kwenye duka la diwani huyo, tumefanikiwa kukamata bangi kiasi cha robo kilo. Ni bangi kavu ambayo imeshaandaliwa tayari kwa ajili ya kufanya packing na kuuzwa,” alisema Kamanda Kyando.

Akizungumzia silaha aina ya gobole waliyoikuta nyumbani kwa diwani huyo anayodaiwa kuimiliki kinyume cha sheria, alisema ingawa ni silaha ya kizamani ina nguvu ya kuua tembo.

“Silaha hii ina nguvu sana, ina uwezo wa kuua tembo na ni hatari sana akipigwa binadamu kwa silaha hii. Kwahiyo msiione hapa mkaidharau, ina nguvu sana,” aliongeza.

Kamanda Kyando aliwataka viongozi wote waliopewa dhamana na wananchi kutotumia nyadhifa zao kufanya uhalifu. Alitoa wito wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kufichua uhalifu bila kujali waliofanya uhalifu huo.

Serikali Yaiamuru Bodi ya Mikopo Istishe Makato na Imlipe Pesa Zake Mstaafu Aliyekuwa Akikatwa Kimakosa

$
0
0
Serikali  imeiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kusitisha mara moja makato ya fedha yaliyokuwa yakifanywa kwenye malipo ya pensheni ya mstaafu Ernest Lameck, katika Chuo cha Ualimu cha Tukuyu kilichopo wilayani Rungwe.

Agizo la kusitishwa kwa makato hayo limetolewa baada ya kubainika kuwa deni hilo ni hewa kwa kuwa mtumishi huyo mstaafu hakuwahi kusoma katika chuo cha Elimu ya Juu.

Amesema Bodi ya Mikopo imekuwa ikitoa mikopo na kwamba kinachofanywa na taasisi hiyo ya Serikali ni wizi.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ametoa agizo hilo jana alipofanya ziara katika Chuo cha Ualimu Tukuyu na kuelezwa juu ya uwepo wa mstaafu huyo ambaye amekuwa akikatwa fedha wakati si mnufaika wa mkopo.

Mkuu wa chuo hicho, Ubaya Salumu, amemweleza Waziri kuwa Lameck aliyekuwa mtumishi chuoni hapo alianza kukatwa fedha kwenye pensheni yake na alipofuatilia alibaini kuwa makato yamekuwa yakifanywa na Bodi ya Mikopo.

Amesema jambo la kushangaza ni kuwa kabla na wakati wa utumishi wake, Lameck hakuwahi kusoma elimu ya juu ambayo angeweza kuomba mkopo kutoka katika bodi hiyo.

Lameck amebainisha kuwa baada ya kufuatilia alibaini kuwa Bodi ya Mikopo inamdai Sh milioni tisa na ni kwa muda mrefu amejaribu kufuatilia jambo hilo pasipo mafanikio.

Kutokana na hali hiyo, Profesa Ndalichako mbali na kuiagiza bodi kusitisha makato hayo mara moja, pia aliagiza fedha zote alizokatwa mtumishi huyo zirejeshwe ili anufaike na stahili zake.

“Haiwezekani mtu haukukopeshwa halafu waanze kumkata. Hili nataka lifanyike haraka na si tu kusitisha makato, bali lazima Bodi wakulipe fedha zako zote walizokukata,” alisisitiza.

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Kwa Umma Kutoka Mkoa Wa Mwanza

$
0
0
Tarehe 12.10.2016 majira ya saa 16:35 katika eneo la Busenga “A” kata ya Buswelu wilaya ya Ilemela jiji na mkoa wa Mwanza, askari walifanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Juma Biria miaka 42, mfanya biashara na mkazi wa mtaa wa Busenga akiwa na vifaa vya kutengeneza noti bandia ambavyo ni kemikali ikiwa ndani chupa kubwa, sabuni ya maji iliyowekwa ndani ya chupa ndogo, karatasi zilizokatwa mfano wa noti ya shilingi elfu kumi pamoja na unga ambao bado haujafahamika ni wa kitu gani, kitendo ambacho ni kinyume na sheria na taratibu za nchi .

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu akishirikiana na wenzake amekuwa akifanya shughuli hiyo ya uhalifu, ndipo zilipatikana taarifa za kiintelejensia kuhusiana na uhalifu huo, ndipo askari waliweza kufuatilia na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa huyo.

Aidha kwa sasa jeshi la polisi lipo katika mahojiano na mtuhumiwa, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili hatua  stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake. Aidha jitihada za kuwasaka wenzake wanaodaiwa kushirikiana na mtuhumiwa huyu katika uhalifu huo bado zinaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa rai kwa wakazi wa jiji na mkoa wa Mwanza, akiwataka kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na wahalifu wa aina kama hii, ili waweze kufikshwa katika vyombo vya sheria, kwani jeshi la polisi linaamini endapo wananchi wataendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lao, tutaweza kukomesha uhalifu katika mkoa wetu.

imetolewa na:

DCP: Ahmed Msangi
Kamanda wa polisi (m) Mwanza

Ubunge wampita Kushoto baada ya Mahakama ya Rufaa Kutupilia Mbali Maombi Yake

$
0
0
Hatimaye mbio za David Kafulila kupinga mahakamani matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa Kigoma Kusini ya Oktoba mwaka jana uliompa ushindi Husna Mwilima (CCM) zimefika ukingongoni baada ya mahakama ya rufaa kutupilia mbali maombi yake.

Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa waliokaa mjini Tabora, jana lilitoa maamuzi yake kuhusu rufaa ya Kafulila na kueleza kuwa wameyatupilia mbali maombi hayo kwakuwa yamekosa nguvu yenye uhalali wa Kisheria.

Aidha, Mahakama hiyo ya Rufaa imemtaka Kafulila ambaye hakuhudhuria mahakamani hapo, kulipa gharama zote za shauri hilo la madai namba 212 la mwaka 2016.

Akizungumza baada ya maamuzi hayo ya Mahakama ya Rufaa, Mbunge wa Kigoma Kusini, Mwilima alisema Kafulila alijua kuwa hakuwa na madai yoyote mahakamani na kwamba alicholenga ni kumsumbua ili akose muda wa kuwatumikia wananchi wake.

“Kafulila alijua fika kuwa hakuna kesi ya yeye kukata rufaa. Lakini alikata rufaa kunisumbua ili nikose muda wa kuwatumikia wananchi waliniingiza bungeni,” alisema Mwilima.

Kafulila alifungua shauri la madai namba 2 la mwaka 2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, akipinga ushindi wa Mwilima. Katika shauri hilo, Kafulila aliwalalamikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msimamizi wa uchaguzi na Husna Mwilima.

Mahakama Kuu iliyatupilia mbali maombi ya Kafulila ya kutaka kutengua ubunge wa Mwilima ndipo Mbunge huyo wa zamani wa Kigoma Kusini alipoamua kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa ambayo ni Mahakama ya juu zaidi nchini.

Kesi hiyo iliyovuta umakini wa wananchi wengi jimboni humo na huenda ndio kesi ya uchaguzi iliyovuta watu wengi zaidi tangu kumalizika kwa uchaguzi wa mwaka jana, imefikia ukingoni kwa kuhalalisha ubunge wa Mwilima.

Mtanzania Aliyekamatwa Kwa Ugaidi Kenya Apata Ugonjwa wa Akili

$
0
0
Raia wa Tanzania aliyeshtakiwa kwa kuhusika katika shambulio la kigaidi la chuo kikuu cha Garissa 2015 ambapo takriban watu 149 waliuawa amepata ugonjwa wa kiakili akiwa jela.

Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya, Rashid Charles Mberesero aligunduliwa kuwa hawezi kuendelea na kesi baada ya ripoti ya daktari wa maswala ya kiakili kusema kuwa amekuwa akitibiwa tatizo la kuwa na ''mienendo isiyo eleweka'' katika jela ya kamiti.

Gazeti hilo linasema kuwa ameshtakiwa pamoja na Mohamed Ali Abdikar, Hassan Aden Hassan, Sahel Diriye na Osman Abdi.

Washukiwa hao wote wamekana mashtaka 162 ya ugaidi.

Kulingana na Daily Nation, siku ya Jumatano, upande wa mashtaka ulitaka kupewa muda kujadiliana jinsi ya kuendelea na kesi hiyo dhidi ya wenzake kutoka Kenya.

Matokeo ya ripoti ya ukaguzi wa akili iliowasilishwa katika mahakama ilisema kuwa alidungwa sindano yake ya kila mwezi mnamo tarehe 12 mwezi Septemba.

''Amekuwa akikabiliwa na matatizo yasio ya kawaida, ambapo anaamini watu wote karibu naye wana nia za kishetani'', daktari Mucheru Wang'ombe aliandika katika ripoti hiyo.

Kulingana na Daily Nation, daktari huyo amesema kuwa mshukiwa huyo anahitaji matibabu na uchunguzi wa kila mara wa akili yake.

''Ripoti hiyo inasema kuwa mshukiwa huyo apewe matibabu katika hospitali ya Mathare kila mwezi na hayuko katika hali ya kuweza kuendelea na kesi hiyo na kwamba majadiliano yanaendelea'', alisema kiongozi wa mashtaka Eddie Kadebe.


Picha: Tunda Man Afanya ‘Send-off’ na Mrembo Huyu

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man pamoja na mpenzi wake wa muda mrefu wamefanya ‘send-off’ wakijiandaa kuingia katika maisha ya ndoa.

Alhamisi hii usiku zilisambaa picha katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha Tunda Man pamoja na mpenzi wake wakiwa kwenye ‘send-off’.

Mmoja kati ya wasanii ambao walihudhuria shughuli hiyo ni Dojo Janja ambapo alimpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo.

“From❤️ congrats my big brother captain @tundamantz. Kesho tunabeba jiko letu mapema mapema tu, hatucheleweshi mambo. Mimi ninao wengi sijui nioe yupi,” aliandika Dogo Janja Instagram.

Wiki chache zilizopita, muimbaji huyo wa wimbo ‘Mama Kijacho’, aliiambia Bongo5 kuwa atafunga ndoa hivi karibuni.

“Kusema kweli suala la kuoa naoa hivi karibuni. Kwa hiyo mtu yeyote anakaribishwa na nipo tayari kuingia kwenye maisha ya ndoa,” alisema Tunda Man.


TCRA yapiga ‘Stop’ Simu za Samsung

$
0
0
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepiga marufuku uingizaji na usambazaji wa simu za mkononi za Smartphone Samsung Galaxy note 7 kwa kuwa zina matatizo ya betri.

TCRA pia imewataka wananchi ambao tayari wanatumia simu hizo kuzizima na kuzirudisha haraka katika maduka walikozinunua.

Akizungumza na MTANZANIA   Dar es Salaam jana, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy, alisema watanzania wajihadhari kuitumia simu hiyo kwa kuwa Kampuni ya Samsung yenyewe imeiondoa sokoni.

“Simu hiyo tayari Samsung wenyewe wamesema ina matatizo ya betri na mara mbili sasa imelipuka,” alisema Mungy.

Aliwaomba watu wenye simu za aina hiyo kuzirudisha madukani haraka wabadilishiwe ama kurudishiwa fedha zao.

“Hata kama uliletewa zawadi kutoka nje ya nchi nawaomba warudishe huko   kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza,” alisema Mungy.

Hivi karibuni simu aina hiyo iliyothibitishwa na kampuni hiyo kuwa ilikuwa salama, ilishika moto kwenye ndege nchini Marekani.

Simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa mikononi mwa abiria aliyekuwa kwenye shirika la ndege la Southwest Airlines.
Shirika hilo liliwaondoa kwa dharura abiria waliokuwa kwenye ndege  iliyokuwa imepangiwa kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi Baltimore, Maryland muda mfupi kabla ya kupaa.

Donald Trump Ashtukia Mchezo...Adai Shutuma za Kukashifu Wanawake ni Njama Alizotengenezewa

$
0
0
Mgombea urais wa chama cha Republican Marekani Donald Trump amewaambia wafuasi wake kuwa shutuma za kukashifu wanawake ni njama ya kumfanya ashindwe uchaguzi wa Marekani.

Katika mkusanyiko na wafuasi wake huko Florida Trump amekanusha kuwa tuhuma hizo ni uongo.

Ikiwa zimebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo Trump anaonekana kushindwa dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton.

Mapema mke wa Rais bi Michelle Obama amemshambulia Trump na kusema kuwa kitendo cha Trump cha Udhalilishaji wa wanawake ni cha Kushangaza na kutisha.

Mke wa Rais wa Nigeria Aisha Buhari Ampiga Mkwala Mzito Mumewe.....

$
0
0

Mke wa Rais, Aisha Buhari amemuonya mumewe kuwa hatomuunga mkono katika uchaguzi ujao kama hatafanya mabadiliko katika Serikali yake.
Aisha Buhari amesema mumewe "hawafahamu" wengi wa maafisa wakuu aliowateua serikalini na akadokeza kwamba Serikali imetekwa.

Amesema kuwa "watu wachache" ambao huamua ni nani watateuliwa.

Ester Bulaya Kuwekwa Kikaangoni Jumatatu

$
0
0
ESTER Bulaya, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, mkoani Mara anatarajia kupanda kizimbani Jumatatu ya tarehe 17 Oktoba, mwaka huu ili kutoa ushahidi wake katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge inayomkabili, anaandika Charles William.

Bulaya atalazimika kuhojiwa na kujibu maswali ya mawakili wa upande wa walalamikaji kwa upana zaidi baada ya kiapo chake kuingizwa katika kumbukumbu za Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza.
Hatua hiyo inakuja baada ya Jaji Noel Chacha wa mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na Costantine Mutalemwa, wakili wa waleta maombi ambaye alikuwa akiomba baadhi ya aya zilizopo katika hati ya kiapo cha Bulaya zifutwe.

Tundu Antiphas Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ndiye wakili wa Bulaya katika kesi hiyo ambapo amepiga kambi mkoani Mara kwa takribani wiki mbili sasa wakati shauri hilo likiendelea.

Katika kesi hiyo namba moja ya mwaka 2015, walalamikaji ni watu wanne wakiongozwa na Magambo Masato, watu hao wamejitambulisha kama wapiga kura katika jimbo la Bunda Mjini huku Steven Wassira, aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa walalamikaji.

Tanzania Yajitoa Katika Mpango wa Visa ya Pamoja Afrika Mashariki

$
0
0
Tanzania imejitoa katika mpango wa Visa ya pamoja unaohusisha mataifa ya Kenya, Uganda na Rwanda. Mpango huo uliadhimia kushirikisha mataifa yaliyo katika mpango wa Viza ya pamoja katika kutanga biashara ya utalii kwa pamoja.

Aidha Tanzania pia haitashiriki katika matukio ya kitalii ya Afrika Mashariki unaoendeshwa na mataifa hayo jirani.

Katibu wa baraza la utalii Najib Balala amesema Tanzania imejiondoa katika mkakati huo kwasababu inahofia ushindani kutoka Kenya.

=========
Tanzania has dealt Kenya another blow by distancing itself from the common visa launched between Kenya, Uganda and Rwanda.

The common visa is meant to, among other things, enable the members states to jointly market their tourism as a single product.

Tanzania also wants nothing to do with the joint marketing strategies pushed by Kenya, Uganda and Rwanda and will not participate in the East African tourism platform events being pushed for by the neighbours.

The joint visa has been issued to 4,000 tourists who will be visiting the three countries, now dubbed ‘the coalition of the willing’.

In a media briefing Wednesday, Tourism Cabinet Secretary Najib Balala said Tanzania was wary of competition from Kenya.

“Tourists who will be moving between the three countries that form the coalition will now be using a common visa that will be charged at $100 (Sh10,122) instead of $150 (Sh15,183) that each country charged before,” Mr Balala said.

“The coalition of the willing has also agreed to have a common East Africa stand at the world Travel Market to be held in London on November 7. The stand has been dubbed ‘borderless East Africa’, but Tanzania will not be part of it,” he added.

However, Balala asserted that if the three East African countries want to move on with a regional cooperation pact on tourism, nothing will stop them and hoped the latest joint strategy will motivate Tanzania to join in.

Balala said the problem with the East African region is that countries live with “a fear of the unknown”. He called on the country’s neighbours to look at each other not as competitors, but as friends complementing each other. “Our competitors are the Caribbean countries and the Far East. We shouldn’t compete among ourselves,” Balala said. “I want to encourage Tanzania to join us. Our doors are open,” he added.

At the same time, the CS gave the numbers of tourist arrivals from the region, which indicated Tanzania’s numbers had shrunk compared to Uganda.

“From Uganda, we had 50,000 arrivals. From Tanzania we had 30,000, while we had 25,000 from Ethiopia. We are yet to get numbers from Rwanda and Burundi,” Balala said.

The latest development comes just months after Tanzania declined to sign the Economic Partnership Agreement (EPA) between EAC and European Union (EU).

Source: Standard Digita

Mganga Afunguka " Ali Kiba Kuzimiwa Mic Mombasa ni Tukio la Kishirikina"

$
0
0

Tukio la msanii wa muziki wa Bongo Fleva, kuzimiwa kipaza sauti wakati aki perform jukwaani,hapa mjini Mombasa, limeusishwa na imani za kishirikina.


Akifanya mahojiano na kituo kimoja cha radio nchini Kenya, Mganga mashuhuri wa jadi kutoka nchini Tanzania, aitwaemuungu wa kabili, alinukuliwa akisema kuwa “ Suala la Ali Kiba ni suala la kichawi “, asisingiziwe Sallam meneja wa Diamond wala Diamond mwenyewe, wala waandaaji wa tamasha, wala walinzi wa Chris Brown.


Muungu wa Kabili ambae inadaiwa, alikuwa akiongoza kikosi cha jadi kinachoundwa na waganga mbalimbali kutoka nchini Tanzania na Kongo ya mashariki, alikuwepo jijini Mombasa, kuongoza kamati ya ufundi katika kuhakikisha tamasha hilo linafanyika bila kutokea kwa shari yoyote inayo weza kusababishwa na wachawi au maadui kama vile kunyesha kwa mvua ya kichawi, kutokea kwa stampede ( kiwewe kinachopelekea watu kukanyagana na kufa ), nakadhalika.


Lakini hata hivyo alipoulizwa kuhusu jambo hilo hakukubali wala kukataa ingawa anasema alikuwepo jijini Mombasa kwa kikazi na alikuwa mmoja wa watu walio hudhuria tamasha hilo.


Muungu wa Kabili aliongeza “ Wachawi na washirikina wanapenda sana kuhudhuria kwenye matukio yenye kuhusisha idadai kubwa ya watu kama vile matamasha ya muziki, mikutano ya kisiasa nakadhalika, kwa saabu katika maeneo hayo, kuna vitu vingi sana vya kichawi na kishirikina ambavyo wachawi huvichukua kwa ajili ya matumizi ya shughuli zao za kichawi “


“Mfano wa mambo ambayo wachawi huyafuata kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu ni pamoja na mchanga, udongo pamoja na mabaki ya vitu vilivyopo katika eneo la tukio.” Aliongeza muungu wa kabili.


Mchanga ama udongo wa kwenye eneo lenye mkusanyiko mkubwa wa watu ambao wamekesha hadi asubuhi huchanganywa na dawa zingine za kichawi kwa ajili ya kutengeneza ndumba za biashara na kufanyab biashara zitoke sana.


Ilhali uchafu uchafu na mabaki ya kwenye eneo lenye mkusanyiko mkubwa wa watu, hutumiwa na watu wa mazingaombwe kwa ajili ya kutengeneza viini macho. Alieleza muungu wa kabili.


Akizungumzia kuhusu tukio la Ali Kuzimiwa kipaza sauti na kushushwa jukwaani bila ridhaa yake, muungu wa kabili alisema.


“ Uzuri ni kwamba, nilikuwepo katika eneo la tukio na nilishuhudia kila kitu. Katika mikusanyiko mikubwa ya watu ambayo inakesha huwa kuna shughuli nyingi sana za kichawi na kishirikina. Kama hauna macho ya kiroho, hauwezi kuona kinacho endelea.”


Una jua katika uchawi huwa kuna vitu vinaitwa “ Mamlaka za kichawi”. Mamlaka za kichawi zinahusisha mambo mengi sana. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na mambo ambayo wachawi huyatumia kulogea watu. Unajua mchawi hawezi kuloga mtu bila kufananisha ulozi wake na kitu kingine.


Kwa mfano , katika uchawi wa kuwatenganisha watu kama vile wanandoa, ndugu au marafiki, na kuwa fanya wasionane tena hadi wanarudi kaburini, wachawi hufanya matambiko maalumu, kasha hutafuta nyayo za watu walio kusudia, nyayo hizo zinafanyiwa ulozi, halafui unyayo wa mtu mmoja utakwenda kuzikwa kwenye mlima mmoja, ambao labda upo Mombasa, na unyayo wa mtu mwingine utaenda kuzikwa kwenye mlima ambao labda upo, NAIROBI.


Sasa katika ulozi wao, wachawi watasema maneno kama vile “ FULANI BIN FULANI, SIKU YA LEO NIMEKUZIKA, KATIKA MLIMAA HUU ULIOPO HAPA MOMBASA, NA FULANI BIN FULANI YEYE AMEZIKWA KWENYE MLIMA FULANI ULIOPO HUKO NAIROBI. KAMA MLIMA HUU ULIOPO HAPA MOMBASA, UNAWEZA KUKUTANA NA MLIMA ULIOPO NAIROBI, BASI NA WEWE FULANI BIN FULANI AMBAE NIMEKUZIKA KATIKA MLIMA HUU, UTAWEZA KUKUTANA NA FULANI BIN FULANI AMBAYE YUPO NAIROBI.


LAKINI KWA KUWA WEWE FULANI BIN FULANI AMBAE UMEZIKWA KWENYE HUU MLIMA ULIOPO HAPA MOMBASA, HAUWEZI KAMWE KUKUTANA NA FULANI BIN FULANI, AMBAE AMEZIKWA HUKO NAIROBI.BASI HATA W EWE FULANI BIN FULANI HAUTAKUTANA NA FULANI BIN FULANI MPAKA SIKU UNAINGIA KABURINI “


Mifano ipo mingi sana. Haya mambo ya kulinganisha katika ulozi yapo ya aina mbili, Yapo ya asili na yapo ya kutengeneza.


Turudi kwa Alikiba na kuzimiwa kipaza sauti Mombasa. Kwenye mikusanyiko ya watu wengi, wachawi hutuma majini kwa ajili ya kuwaangusha au kuwaua watu, na kisha baada ya hapo, kutumia udongo , au mabaki yaliyopo katika eneo husika, katika kutengeneza uchawi wa aina mbalimbali kama vile kifafa cha kichawi, au kushusha nyota.


Uchawi huu hutumwa katika eneo husika, na hunuizwa watu kuanguka,kuzimia au hata kufa. Walengwa wakuu wa uchawi huu ni watu maarufu.


Tukio la Ali Kiba, katika ulimwengu wa kiroho lina ashiria, kuzimwa na kushushwa nyota yake kwa nguvu.

Kuzimiwa kipaza sauti kunaashiria kuzimwa kwa nyota yake na kushushwa jukwaani kuna ashiria kushushwa nyota yake.


Tukio hili halikukusudiwa kwa Ali Kiba, ni uchawi ulionuiziwa kwa watu wote katika eneo hilo, sema Ali Kiba amekuwa mhanga tu.

Hii maana yake ni kwamba, wachawi wataenda kuchukua mchanga katika eneo hilo, na watautumia kutengeneza uchawi wa kushusha na kuzima nyota za watu.


Siku ya tukio, sio Ali Kiba pekee, wapo watu wengi tu walio anguka tena wenyewe, lakini kwa sababu sio maarufu, Ali Kiba ndio alionekana.


Hii haimaanishi kuwa Ali Kiba ameshushwa nyota yake la hasha. Nyota yake itaendelea kuwa juu na ataendelea kufanya vizuri katika shughuli zake za muziki.


Wachawi watatumia tukio la kushushwa na kuzimiwa kipaza sauti. Kwa mfano “ Kama fulani bin Fulani, pamoja na kwamba yupo juu , lakini alizimiwa kipaza sauti na akashushwa chini, basi hata Fulani bini Fulani nae pia nyota yake itazimwa na kushushwa.


Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa taarifa kwamba meneja wa Salam ndio alifanya fitna ili Ali Kiba azimiwe microphone pamoja na madai kwamba, walinzi wa Chris Brown ndio walishinikiza Ali Kiba ashushwe,muungu wa akili alisema.


“ uchawi ni unafiki. Hizo sababu unazo zitaja ni unafiki na sio kweli. Wachawi hutumia busara sana wanapo fanya mambo yao, siku zote huwa hawataki kujulikana ndio maana huwa wanatengeneza sababu mbadala, ili watu wasiwastukie.


Mfano wakitaka kukuchukua msukule, watakutengenezea sababu kama vile ajali au ugonjwa wa ghafla nakadhalika.


Mfano mzuri ni ule wa kwenye maandiko matakatifu, Ndugu zake Yusufu mwana wa Yakobo, walipo muuza ndugu yao utumwani, walitengeneza uongo wa kupeleka kwa baba yao kwamba, Yusufu ameuwawa na Simba.


Katika kusapoti uongo wao, wakararua nguo za Yusufu, wakachinja damu ya kondoo na kupaka kwenye nguo za Yusufu.


Baba ya Yusufu alivyo tazama nguo za mwanae zilizo tapakaa damu, akaamini kabisa motto wake amekufa, kumbe ameuzwa utumwani. Hiyo ndio hekima ya kishetani inayo tumiwa na wachawi.


NINI SULUHISHO KWA ALIKIBA : muungu wa kabili anasema “ Katika ulimwengu wa kiroho, Ali Kiba haja athiriwa chochote na tukio la Mombasa, lakini ni muhimu awatafute masheikh, wamfanyie kisomo maalumu na ibada..


Miezi kadhaa iliyo pita, mwanadada mmoja alitoa ushuhuda wake kupitia vyombo mbalimbali vya habari, akimlaumu muungu wa kabili kwa kumfanyia madawa ya kichawi ambayo yalimletea matatizo makubwa katika maisha yake.


Maelezo ya mwanadada huyo yalibeba kichwa “ NILIMLISHA MUME WA MTU LIMBWATA LA NYAMA YA BUNDI “ na yanapatikana mtandaoni.

Zitto Kabwe Afunguka Haya Kuhusu Hayati Mwalimu Nyerere.......

$
0
0

Kuipitia ukurasa wake wa Facebook Zitto kabwe ameanza kuandika hivi...

Nyerere wangu mimi!

Mwaka 1984 nilianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kigoma, katika mji wa Kigoma. Nakumbuka kupelekwa Shule siku ya kwanza na mama yangu mzazi Bi Shida Salum (Mungu amrehemu) nikiwa sina viatu yaani pekupeku wala begi la mkononi, nilikuwa nimebeba mfuko wa nailoni. Nakumbuka usiku wa kuamkia siku ya kwanza kwenda shule, sikulala kwa furaha na hamu ya kuwa msomi, nilijisikia fahari kuanza shule japokuwa sikuwa na kitu chochote cha zaida zaidi ya kaptula ya shule na shati liloshonwa kwa kitambaa cha sanda. Pia nilianza shule nikiwa nimechelewa kwa mwaka mmoja maana wenzangu walianza wakiwa na miaka 7. Mwaka 1983 nilipopelekwa shule mkono wangu haukuweza kushika sikio upande wa pili, ambacho kilikuwa kipimo cha kuandikishwa darasa la kwanza.

Hali ya maisha wakati huo ilikuwa mbaya sana. Nakumbuka kwenda shuleni nikiwa sina kitu tumboni au siku nzima nilikunywa uji usio na sukari. Uji wenyewe ulikuwa ni wa unga wa njano uliotokana na mahindi ya njano ambayo tuliambiwa nchi yetu ililetewa kama msaada kutoka nchini marekani.

Shule yetu kama zilivyokuwa shule nyingi za wakati huo hatukuwa na madawati ya kutosha na vyumba vya madarasa vilikuwa vichache sana. Ilikuwa ni kawaida kwa wadogo (darasa la kwanza mpaka la tatu) kusomea chini ya mwembe na kukaa juu ya matofali. Hali hiyo ilipelekea kaptura yangu ya shule kuwekwa viraka vingi maana ilikuwa inachanika mara kwa mara. Nyakati nyingine ilibidi kwenda shuleni na shati likiwa halijakauka hasa siku za alhamis, siku ya usafi na iwapo nikiwa zamu ya mchana kwani nilikuwa nina shati moja tu tena lililotokana na kitambaa cha sanda.


Kwa dhahiri, watoto wa masikini na matajiri tulikuwa shule moja, darasa moja hata wote kukaa kwenye matofali. Watoto watawala na watawaliwa tulicheza mpira pamoja, kuruka dana na hata kuruka kamba. Hatukujisikia wanyonge kwa sababu hatuna viatu au kuvaa kaptura zenye viraka na mashati ya sanda. Kamwe sikumbuki kudharauliwa shuleni sababu ya uduni wa maisha yangu. Heshima ilitokana na uwezo wako darasani na kupitia hilo nilipata marafiki wa kutoka madaraja yote ya maisha. Nakumbuka mtoto wa Mkurugenzi wa Maendeleo Mkoa wa Kigoma ndugu Daniel Masanja ndiye alikuwa rafiki yangu wa karibu na kwa kuwa sikuwa na hata pesa ya kununua bajia wakati wa mapumziko, yeye alikuwa ananinunulia.


Huko baadaye, ada yangu ya kidato cha kwanza ililipwa na Mzee Sebastian Kasomi ambaye mwanaye Kasomi Mabula alikuwa rafiki yangu mkubwa mara alipohamia shuleni kwetu akitokea mjini Shinyanga. Mzee Kasomi alikuwa Mkuu wa idara ya Kodi ya Mapato mkoani Kigoma.


Licha ya uduni wa maisha watoto wengi tuliishi kwa matumaini makubwa sana. Mwalimu wetu Mkuu ndg. Daniel Andulile alikuwa mkali sana kwa watoto wote bila kujali daraja la maisha la wazazi wao. Alikuwa anatucharaza viboko kwa makosa na utundu bila ubaguzi. Alisisitiza sana kusoma kwa bidii ili kujenga Taifa. Dhana hii ya kujenga Taifa iliingizwa kwenye akili zetu na sisi kumeza bila kujali maana yake. Wakati mwingine tulikuwa tunarudi nyumbani huku tukijadili kitoto kuwa tunajenga Taifa. Kila siku mwendo wa kilometa Sita kwenda na kurudi shuleni.


Elimu hii isiyo ya kibaguzi sasa najua ilitokana na sera za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Jitihada zangu darasani ndio ziilikuwa kipimo cha utu wangu na sio uwezo wa kiuchumi wa wazazi wangu.. Elimu iliyompa fursa sawa za kuendelea na kusonga mbele mtoto aliyekuwa kigoma, kantalamba au Dar es salaam. Elimu iliyokuza ndoto, kuinua ari na kujenga matumaini ya kila mtoto wa kitanzania. Elimu iliyovunja na kusambaratisha matabaka ya kiuchumi na dhamana. Elimu iliyojenga uzalendo na hamasa ya kutumikia taifa letu kwa misingi ya haki, uadilifu na upendo.


Sikuwahi kukutana na Mwalimu Nyerere isipokuwa niliwahi kumwona akiwa ndani ya gari nikiwa nimepanga mstari barabarani alipofanya ziara mkoani kwetu mwaka 1987 nikiwa darasa la nne. Lakini nilikuwa kama ninaishi naye kutokana na namna nilivyotaka kuwa kama yeye. Nikiwa darasa la pili nakumbuka katika mkebe wangu ( mathematical set) mkuu kuu niliweka picha ya kukatwa kutoka kwenye gazeti ya Mwalimu na Kawawa. Na nilijisikia fahari kuwa na picha zao, mara zote nilipokuwa nafungua mkebe kutoa kalamu nilijisemea kimoyomoyo, “siku moja nitakuwa kama wewe”


Licha ya maisha magumu tuliyokuwa tunaishi, maisha ya kupanga mawe kwenye mstari wa kununua mahitaji muhimu kama sukari, sabuni na mafuta kutoka duka la ushirika, maisha ya kushindia uji wa yanga na kutembea mwendo mrefu kwenda shuleni, niliishi kwa imani kubwa kuwa mimi na watoto wengine tupo sawa. Usawa katika kupata elimu, usawa katika kucheza na usawa katika ndoto na matumaini. Nimemaliza elimu ya Chuo Kikuu, ndoto niliyoruhusiwa kuwa nayo kwa sababu ya sera za Ujamaa, za Mwalimu Nyerere.


Ujamaa haukuwa katika usawa wa elimu tu ambapo kila mtoto alipata elimu bure na bora katika Shule za umma bila ubaguzi bali pia namna jamii iliishi. Mtoto alikuwa analelewa na jamii nzima. Ukifanya makosa mtaani mzazi yeyote anakuadhibu ili kukurekebisha. Ukifanya jambo jema, mzazi yeyote anakupongeza.


Mwaka 1985 mwezi Novemba nilipokuwa natoka shuleni, karibia na Benki ya Taifa ya Biashara Tawi la Obed Katikaza, nilikutana na Mama Colleta Furugunya tuliyekuwa tunaishi mtaa mmoja na nikimwita bibi Colleta. Aliponiuliza matokeo yangu ya mtihani wa kumaliza muhula wa pili wa darasa la pili kwa kujiamini nikampa karatasi yangu ya matokeo. Nilikuwa nimeshika nafasi ya tatu darasani nyuma ya Ramadhan Kalukula na Haki Manyaga. Bibi Colleta alinishika mkono mpaka duka la Viatu, Bora Shoes na kuninunulia jozi yangu ya kwanza ya viatu. Viatu vile viliitwa Asante Salim, aliyekuwa Waziri Mkuu wa mwisho wa Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa anajaribu kubadili hali mbaya iliyokuwepo. Hivyo ndivyo nilivyopata viatu vyangu vya kwanza vya shule. Shukrani kwa sera nzuri ya ujamaa, mshikamano na upendo.


Hizo ni enzi.

Maafisa 10 wa Kitengo cha Mabomu ya Nyuklia Marekani Wadai Donald Trump Hana Utulivu wa Kakabithiwa Kifaa cha Ulipuaji Bomu la Nyuklia Akiwa Rais

$
0
0

MAREKANI: Maafisa 10 wastaafu wa kitengo cha ulipuaji wa nyuklia wamepinga Donald Trump kuwa Rais. Wamedai hana utulivu wa kukabidhiwa kifaa cha ulipuaji wa bomu la nyuklia.
Maafisa hao katika barua yao wamesema mtu anayekabidhiwa jukumu hilo zito anatakiwa awe mwenye busara na maamuzi sahihi.

Hatimaye TPA yaruhusu kwa muda mfupi containers kuendelea kupelekwa ICD's

$
0
0
Mnamo Tarehe 10/10 Sumatra walitoa waraka wa kuzuia kontena zote zinazoingia nchini kubaki bandarini hali iliyopekelea sintofahamu kwa wadau wengi wa bandari hasa wamiliki wa meli kupitia kwa mawakala wao hapa nchini na wamiliki wa hizo Icd's hatimae jana 13/10 bandari imeruhusu makasha kuendelea kwenda bandari kavu.

Serikali sasa iachane na kufanya kazi kisiasa iache wataalamu wafanye maamuzi ya kitaalamu.

Download SIASA APP Kusoma zaidi..

Usiyoyajua Kuhusu Nyerere: Shuleni Alikuwa Toto Tundu!, Almanusura Afukuzwe Tabora School

$
0
0
Leo tunapomkumbuka Mwalimu, naombeni niwadokolee machache kumhusu mwalimu ambayo sidhani kama wengi mliyafahamu, na kama wapo ni yale waliyoyafahamu kwa kuyasikia tuu lakini hayajaandikwa popote!.


  • Baba yake alikuwa ni Chifu na alikuwa na wake 22!. Jee unawafahamu ndugu wengine wa Nyerere kwa Upande wa Baba!. Hawa Julius Kambarage Nyerere (JK-Nyerere), Joseph Kizurira Nyerere (JK Nyerere), na John Kiboko Nyerere (JK Nyerere), hawa ni ndugu wa Tumbo moja. Jee ndugu wengine wa Mwalimu kwa hao wake wengine 22 wa baba yake ni kina nani?.
  • Kumbe Mwalimu alibahatika kusoma kwa bahati tuu!. Ndugu wengine wote kwa Baba, ukiachia wa tumbo la Mama yake, waliishia kuchunga mbuzi!.
  • Baba yake, alikataa Ukristo kata kata!. Wamishenari walipomshawishi kuachana na dini asili na kujiunga na Ukristo, aliwauliza Ukristo una nini ambacho dini za asili hazina!. Walimjibu, Upendo, Amani, Unyenyekevu, Utii, Haki etc, aliwajibu tena kwa mifano hai jinsi wanavyohubiri Upendo, Amani, Unyenyekevu, Utii na Haki.
  • Alianza shule akiwa na miaka 12, na darasani alikuwa na akili sana hivyo akarushwa baadhi ya madarasa!.
  • Akiwa Tabora School ndipo alipo pokea Ukristo kwa kubatizwa jina la Julius ambalo alilicopy toka kwa Julius Ceaser!
  • Akiwa Tabora School, alikuwa ni mtoto mkaidi sana!. Adui zake wakuu walikuwa ni ma prefects!. Alishitakiwa mara kadhaa kwa mwalimu mkuu na ukafikia wakati Mwalimu Mkuu akamaamua Julius afukuzwe shule!. Mwalimu wake wa darasa licha ya utundu wake, alimpenda sana kwa sababu alikuwa na akili sana!. Hivyo akamnusuru kufukuzwa shule kwa kumfanya na yeye awe prefect!.

Source ni Mwalimu Mwenyewe katika mahojiano na mwandishi Mzungu yaliyofanyika mwaka 1964 mara baada ya muungano!.

Jee na wewe, kuna yoyote ya mwalimu unayoyajua na hayaandikwa popote, ungependa ku share na sisi?!.

Pasco.

Ninavyoishi na Aunt Ezekiel ni ndoa tosha – Mose Iyobo

$
0
0
Dancer maarufu wa Diamond, Mose Iyobo amesema jinsi anavyoishi na Aunt Ezekiel ni ndoa tosha lakini atafunga ndoa ili watu wa verify kama instagram.
Mose Iyobo na Aunt Ezekiel wamefanikiwa kupata mtoto mmoja [Cookie] mwenye umri wa mwaka mmoja.

Akiongea kwenye kipindi cha E News, kinachoruka kupitia EATV, Iyobo alisema, “Lakini ninavyoishinae ni ndoa tosha kwa sababu tunaishi kama baba na mama hivyo nataka kujithibitisha inabidi nifunge ndoa ili watu wani-verify kama instagram.”

Aidha Iyobo ameongeza kuwa hapendi watu wanavyomzungumzia vibaya mzazi mwenzie huyo wakidai kuwa eti ni mzee kwani angelikuwa hivyo yeye asingelisogea kwa kuwa angelikuwa kama anatembea na mama yake.

Maradona Nusura Azichape na Veron

$
0
0
Mchezo mahsusi kwa ajili ya kuhamasisha amani ulioandaliwa na Papa Francis ulihusisha nyota kadhaa waliostaafu na ambao bado wanacheza akiwemo Ronaldinho, Francesco Totti, Edgar Davids, Hernan Crespo na Bojan Krkic.

Mchezajia nguli wa soka nchini Argentina, Diego Maradona na Juan Sebastian Veron ambao walikuwa kati ya wacheaji ambao walikuwepo mchezo huo ambao ulifanyika siku ya Jumatano nusra wazichape katika mchezo huo wa hisani uliofanyika jijini Rome, Italia.

Wawili hao walikuwa wakitupiana maneno mpaka kufikia hatua ya kutaka kushikana wakati wakielekea nje ya uwanja wakati wa mapumziko.

Maradona inaonekana hakufurahishwa na jinsi Veron alivyokuwa akimchezea ambapo ilibidi azuiwe na beki wa zamani wa kimataifa wa Brazil Cafu pamoja na watu wa usalama wakati akitaka kwenda kumvaa Veron
Viewing all 2111 articles
Browse latest View live